Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw.
Emmanuel Boaz(wa kwanza kulia) akiwaeleza waandishi wa habari(Hawapo
Pichani) sababu zilizopelekea kutoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500, ambapo
alisema noti ya shilingi 500 inatumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila
siku hivyo hupita kwenye mikono ya watu wengi na kuchakaa haraka,noti hizi
hukaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki na
sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa muda mrefu kuliko noti. Katikati ni Mshauri
wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu na Mwisho ni Meneja Msaidizi,
Sarafu Bw. Abdul Dola.
Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw.
Emmanuel Boaz (kulia) na Mshauri wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu
wakiwaonesha waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Toleo jipya la sarafu ya
Shilingi 500 inayotarajiwa kuingizwa kwenye mzunguko kuanzia mwezi Oktoba
2014.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
No comments:
Post a Comment