Serikali
yatoa usajili kwa makampuni 51 ya wakala Binafsi wa Huduma za ajira nchini kati
ya 87 yaliyowasilisha maombi yake kwa Kamishna wa kazi.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es salaam na Msemaji
wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwan Wema wakati wa mkutano na
waansishi wa habari.
Makampuni
yaliyosalia 36 hayakupata usajili kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
kutokidhi vigezo na kukosa nyaraka muhimu. Alisema wema
Akitaja
baadhi ya makampuni yaliyopewa usajili baada ya kukidhi vigezo kuwa ni PA
Ppospect Africa,Delloitte,KPMG Advisory Ltd, People Ltd, HR-Solutions na AGP
Consultants.
Akifafanua
wema amesema kuwa Kampuni au wakala yoyote ambaye hajapata usajili hatoruhusiwa
kufanya kazi ya uwakala binafsi wa huduma za ajira hapa nchini.
Katika
Kushughulikia suala la usajili Wema amesema kuwa Wizara imeandaa kanuni chini
ya sheria ya ukuzaji wa huduma za ajira Na.9 ya mwaka 1999 na kutangazwa
kupitia tangazo la Serikali Na. 232 la tarehe 11 Julai 2014.
Aidha
Wema alitoa wito Makampuni au mtu yeyote anayetaka kufanya shughuli za huduma
za ajira kuzingatia taratibu na kanuni chini ya Sheria ya kukuza Huduma za
ajira Na. 9 ya Mwaka 1999.
Katika
hatua nyingine Wema amesema kwamba ukodishaji wa Huduma (outsourcing of
Services) haujapigwa marufuku bali kilichopigwa marufuku ni ukodishwaji wa watu
(outsourcing of persons) hivyo ni marufuku kwa wakala wa huduma za ajira
kuajira na kukodisha wafanyakazi au kuajiri kwa niaba ya kampuni nyingine na
wakala hao kuwa sehemu ya mahusiano ya ajira yanayoweza kujitokeza baina ya
watafuta kazi na waajiri.
Tarehe
27/1/2014,Waziri wa Kazi na Ajira,Bibi Gaudensia Kabaka alitoa tamko la
Serikali kuhusu uendeshaji wa wakala binafsi wa huduma za ajira nchini, hii
inatokana na Wizara hiyo kupokea malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kuhusu
utaratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na
baadhi ya wakala binafsi wa huduma za ajira nchini
No comments:
Post a Comment