Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF na wadau
wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi wameanza Mkutano wa kupitia mafanikio
na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini,PSSN unaoratibiwa
na Mfuko huo nchini.
Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango huo
unaowahusisha wataalamu mbalimbali kutoka Taasisi za Fedha na mashirika ya
misaada ya kimataifa utawawezesha pia wataalamu hao kutembelea maeneo kadhaa ya
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini
katika mikoa y Dodoma, Lindi na Zanzibar.
Akitoa tathmini ya utekelezaji wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema tayari kiasi cha
zaidi ya shilingi Bilioni 13 kimetumika katika kutoka ruzuku kwa walengwa wa
Mpango huo na kuwa katika maeneo ambako ruzuku hiyo imetolewa kumekuwa na
mafanikio makubwa ya uboreshaji wa maisha ya kwalengwa wa mpango huo.
Kwa Upande wao wadau wa Maendeleo kutoka BENKI
YA DUNIA , UNICEF,ILO, UNPF,na DFID,,wameonyesha
kuridhishwa kwao na namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini
na kuonyesha kuwa kazi hiyo itakamilimka kwa mafanikio makubwa .
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana
Ladislaus Mwamanga akiongoza Mkutano wa wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF juu
ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru Kaya maskini nchini ,PSSN ulioanza leo Jijini
DSM.
Baadhi ya wadau wa Maendeleo wakiwa katika
mkutano wa kutathmini utekelezaji wa shughuli
za Mpango wa kunusuru Kaya Maskini, unaoratibiwa na TASAF.
Baadhi ya wadau wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakiwa katika mkutano
wa kutathimini utekelezaji wa mpango wa Kunusuru kaya maskini PSSN.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakiongozwa na
mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, aliyevaa tai
walipotembelea chumba cha kurekodi takwimu za walengwa wa mpango wa
kunusuru kaya maskini ambacho kimefungwa
zaidi ya kompyuta 100.
No comments:
Post a Comment