SEMINA
ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na
burudani za Serengeti Fiesta 2014, leo imeendelea kwa kuwapatia dira ya
maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za
kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Shinyanga mjini ndani ya Ukumbi wa Shule ya
Sekondari ya Uhuru iliyopo mjini humo.
Semina
hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu
na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wengi wao wameonesha
hali ya kuelewa baadhi ya mafunzo na mbinu hizo na kuaahidi kuzifanyia
kazi ipaswavyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Msanii
wa Bongo Fleva, Lammeck Ditto, pia alipata fursa ya kusimulia baadhi ya
maisha aliyopitia na kuwataka wakazi wa Shinyanga waendelee
kujitathimini na kujiamini kwa kila hatua wanayoipiga katika kujikwamua
kwenye maisha yao ya kila siku.
Baadhi ya Wahudhuriaji wakiwa kwenye semina hiyo ya fursa.
Mtangazai wa Clouds FM, Shafi Dauda hakuwa nyuma kuzungumza na wanamichezo wa Shinyanga na kuwaonyesha fursa zinazopatikana kupitia michezo.
Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’, Bernard
Munubi ambaye aliwapatia mbinu za mafanikio na namna ya kujikwamua
kiuchumi kupitia mashine za Max Malipo ambazo kwa kiasi kikubwa sasa
zimeweza kuwapatia ajira wakazi wengi nchini.
Naye
mzungumzaji kutoka kampuni ya GSI Tanzania,Afisa Mwanadamizi wa
kampuni hiyo Tanzania,Pius Mikongoti akizungumza kwenye semina hiyo ya
fursa ikiwemo na kuwapa mbinu za kujikwamua kupitia kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment