Tanzania:
Umoja wa katiba ya wananchi nchini Tanzania-UKAWA- uliolisusia Bunge
maalum la katiba tokea mwezi Aprili, leo ulikuwa na mkutano na waandishi
habari .
Madhumuni ya mkutano huo ni kueleza msimamo wa UKAWA kuhusu yalioafikiwa
katika mazungumzo kati ya viongozi wa vyama vya kisiasa vinavyoundwa
kile kinachojulikana kama Kituo cha Demokrasia Tanzania na Rais jakaya
Kikwete kuhusu mkwamo uliojitokeza baada ya Ukawa kujitoa kwenye Bunge
la katiba. Msimamo wa ukawa unafuatia maelezo yaliotolewa jana na
Mwenyekiti wa Kituo hicho mbunge John Cheyo kuhusu matokeo ya mkutano
wao na Rais Kikwe
Mohamed Abdul-Rahman amezungumza na katibu wa UKAWA Julius Mtatiro na
kwanza anaelezea juu ya msimamo wao. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza
alama ya spika za masikioni hapo chini.
No comments:
Post a Comment