Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akiongea wakati wa kufunga
mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yaliyoshirikisha zaidi
ya wajasiliamali 3500 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa
mwakilishi wa Exim Bank Agnes Kaganda baada ya benki hiyo kushinda
nafasi ya tatu kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa
mwakilishi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Badru Idd baada ya benki
hiyo kushinda nafasi ya pili kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha
na uwekezaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda akikabidhi kikombe kwa
mwakilishi wa CRDB Albert Michael baada ya benki hiyo kushika nafasi ya
kwanza kwenye mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
======== ======= =======
Dar es
Salaam. Mafunzo na Kampeni za uhamasishaji nchini Tanzania zitachangia
katika kuongeza kasi ya kufanikisha azma ya kutekeleza mpango wa Taifa
wa Huduma Jumuishi za Kifedha.
Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk
Abdallah Kigoda wakati akifunga Mafunzo ya Wiki ya Huduma za Kifedha na
Uwekezaji katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Semina
hiyo iliyoshirikisha wajasiliamali 3,500 kutoka sehemu mbali mbali
nchini iliratibiwa na Kampuni ya NUEBRAND na kufadhiliwa na wizara ya
viwanda na biashara, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, taasisi ya
PESCODE, Tanzania Standard Newspapers, Sayona, Times FM na Kampuni ya
Ulinzi ya Kiwango.
Alisema shughuli hizo zinasaidia kusogeza huduma karibu na jamii ya Watanzania ambao wote kwa viwango balimbali ni wawekezaji.
“Wengi wanafikiri wawekezaji ni wakubwa tu.Hapana. Wakulima, wajasiriamali hata wamachinga pia,” alisema Waziri Kigoda.
Alisema
kuwa muhimu ni kuwa na uongozi unaoratibu shughuli hizo na kuzingatia
nidhamu ya kujua uongozi uliopo.“Hali hii itapunguza matatizo mengi
yanayoendelea sasa kwa wamachinga,” alisema Waziri Kigoda.
Aidha,
Dk Kigoda aliongeza akisema wafanyabiashara wote, kwa viwango vyao
tofauti wanategemeana kuanzia wamachinga mpaka ngazi ya mitaji mikubwa.
Alisema
ili kufikia hali hiyo, wawekezaji wa makongamano, mafunzo na kampeni
husika ipo haja ya kuendelea kutumia mitandao na mifumo ya teknolojia
mbalimbali katika kuelemisha namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa
wawekezaji wanaoshiriki katika minyororo ya kuongeza thamani.
“Katika
thamani hizo kuna bidhaa za kilimo, ufugaji, madini, misitu, uvuvi hasa
vijijini na hata sekta ya huduma inayojumuisha utii, afya na elimu,”
alisema na kuongeza: “Niwaambieni na kuwafahamisha kuwa moja ya malengo
ya Sayansi ni kubuni na kuunda teknolojia na utaratibu wa kufanya kazi
zenu ili kutumia mali ghafi na nguvu kidogo, kupata vingi kutoka
vichache, kwa manufaa ya taifa.”
Ili
kuhakikisha tekinolojia inaleta ufanisi, Waziri Kigoda alisema, ni
muhimu sana kujikita katika matumizi bora na fursa zinazojitokeza
kupitia teknmolojia. “Wito wangu ni kwa taasisi za fedha, na zile za
utafiti na sayansi kuendelea kushirikiana na serikali kuona ni jinsi
gani tutaendeleza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kupata huduma
za kifedha kwa watu wengi zaidi,” alisema.
Alisema
takwimu zinaonesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu nchini
wanatumia huduma za fedha za simu, hivyo kama kundi hili likibadilishwa
na wakakubali kuwa wateja wa benki nchini, itaongeza upatikanaji wa
huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Nuebrand Events Company, Abdul Ally, akisema
kuwa kumekuwa na mafanikia sana toka kampeni hii ianze kwani idadi ya
makampuni washiriki yamekuwa yakiongezeka toka 1200 mwaka 2012 mpaka
3600 kwa mwaka huu. “Mafanikio ni makubwa, tumepata pia washiriki toka
mikoani mfano Mbeya. Hali hii inatutia moyo,” alisema.
Alisema
kuwa mwakani uhamasishaji huu utafanyika pia jijini Arusha ikiwa ni
katika mkakati wa kuhakikisha mikoa mbalimbali inafikiwa na huduma hii.
No comments:
Post a Comment