==============================================
DOLA ZA KIMAREKANI BILIONI 3 KUTUMIKA KUANZISHA MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA.
============================================
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI MBALIMBALI PAMOJA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
VIWANDA VIPYA KUJENGWA ILI KUKABILIANA UPUNGUFU WA SUKARI.
===================================================
WAKONGWE WA TASNIA YA HABARI WAKUTANA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI,SANAA NA MICHEZO.
============================================================
WALIMBWENDE MISS ARUSHA WAJINOA VIKALI,WAAHIDI KULITETE TAJI LA MISS TANZANIA 2016
MeTL Group yatoa msaada wa Mil. 30.7 kwa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili
====================================================
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA DKT.ASHA ROSE MIGIRO OFISINI KWAKE LEO.
BENO AIPANIA TIMU TAIFA.
SARUJI YA WAASHI TEMBO FUNDI YAZINDULIWA LEO.
Kampuni
ya Saruji Lafarge Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa
matumizi ya uashi. Saruji hii inayojulikana kama Tembo Fundi itawapa
wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni pamoja na kupiga
plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia marumaru.
Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na
ndani ina ubora katika kufanya kazi, nguvu kwenye ugundishaji inashika
vizuri na ina umaliziaji bora wenye kuleta matokeo yaliyo bora zaidi
kwenye kujenga tofali, uzio, marumaru na sakafu.
“Ikiwa
imetengenezwa kutokana na uzoefu na utaalamu wa Lafarge kimataifa
katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi kutumia katika kupiga
plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo itamchukua
muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.
Alisema
faida nyingine muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika
gharama kutokana na mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi
ukilinganisha na mfuko wa saruji ya matumizi ya jumla. Kutokana ya
kwamba inafanya kazi vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo
Fundi itawasaidia wajenzi kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Lafarge, Allan Chonjo alisema daima
Lafarge imekuwa ikiwasikiliza wateja wake. Tembo Fundi ndio suluhisho
la mahitaji ya saruji yenye ubora kwani inatumia maji kidogo, inadumu,
haipati nyufa na ina uwezo wa kujenga eneo pana zaidi na kuufanya ukuta
wako ung’ae zaidi.
“Tembo
Fundi inapatikana katika ujazo wa kilogramu 50 na ni ubunifu wetu
katika kurahisisha kazi za uashi. Lafarge imewekeza sana katika utafiti
uliopelekea uvumbuzi wa saruji kama hii ambayo inapendwa na wajenzi
katika masoko mbalimbali kimataifa. Hii ni moja ya dhima zetu za
kuhakikisha tunawapa wajenzi sulhisho maalumu katika kazi zao. Tembo
Fundi itasambazwa katika maduka yetu yote ya jumla na rejareja pamoja na
kwenye kontena zetu za usambazaji.
==============================================
UTT-PID yaiwezesha Manispaa ya Lindi kuvuna Bilioni 2 katika mradi wa viwanja
======================================
WATU WATATU WAUWAWA NA MMOJA KUJERUHIWA JIJINI MWANZA.
=============================================
YANGA YALAANI VITENDO VYA UVUNJIVU WA AMANI NCHINI ANGOLA.
==============================================
KAMPUNI YA WIA GROUP YAKABIDHI PIKIPIKI TATU KWA SERIKALI YA MTAA WA OYSTERBAY JIJINI DAR LEO.
Meneja
mahusiano wa Kampuni ya Wia Group inayojishughulisha na masuala ya
mawasiliano, Abraham Mwapongo(Katikati) akikabidhi vyeti vya manunuzi ya
Pikipiki, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Zefrini
Lubuva(Kushoto) jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Ofisa Operesheni wa
Wilaya ya Kinondoni, Inspeta Msaidizi Samwel Mkama.
======================================================
No comments:
Post a Comment