UTAFITI WA MALARIA KUOKOA MAISHA YA WATANZANIA.
Mkurugenzi
wa Kinga Jeshini, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni
Kanali Charles Emilio Mwanziva akiongea na mwandishi wa habari kutoka
Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani Luis Velarde wakati wa
ziara ya waandishi hao katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT
iliyopo mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa
malaria.
Mtaalamu
wa maabara katika zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo
mkoani Tanga akiendelea na kazi ya kufanya vipimo vya malaria kwa
kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) ambayo majibu yake
hutolewa baada ya dakika 15.
Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa
tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe.
Mtaalamu
wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani
wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani)
walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na
ugonjwa wa malaria.
Familia
ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe
mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa
watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto
ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.

Vijana
wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo
mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa
malaria.(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini,
Prof. James Mdoe ( wa nne kutoka kulia) akisoma hotuba ya ufungaji wa
mkutano wa siku tatu uliokutanisha wataalam wa masuala ya jotoardhi
kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia,
Eritrea, Marekani, New Zealand na Djibouti kwa ajili ya kujadili taarifa
ya mtaalam mwelekezi kuhusu utafiti uliofanywa katika Ziwa Ngozi
lililopo mkoani Mbeya ambapo kuna viashiria vya jotoardhi pamoja na eneo
la Kibiro nchini Uganda.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini,
Prof. James Mdoe (kushoto) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifunga
mkutano huo. Kulia ni Mjiolojia Mkuu kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya
Nishati na Madini, Jacob Mayalla.
Sehemu
ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji
iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia madini, Prof. James Mdoe (hayupo pichani)
No comments:
Post a Comment