Katibu
wa CCM Tawi la Makangira Kata ya Msasani Nd. Epi Fania Ngonyani
akibadilishana mawazo na Balozi Seif akijiandaa na ujumbe wake kuondoka
Bandarini Malindi kurejea Mjini Dar es salaam baada ya kumaliza ziara
yao ya ujirani mwema. Nyuma ya Ndugu Ngonyaji ni Mwenyekiti wa CCM wa
Tawi hilo Ndugu Haroub Othman Mberwa.

Shirika la ndege la Etihad latoa taarifa kuhusiana na msukosuko wa Ndege yake Indonesia.
Vile vile walikutana na wanafamilia kadhaa wa majeruhi na
kuthibitisha kuwa shirika la ndege la Etihad litagharamia gharama zote
za matibabu.
Kati ya majeruhi tisa ambao walikuwa wamelazwa, wengi wao
wataruhusiwa kuondoka leo. Rais wa shirika la ndege la Etihad na
Mkurugenzi Mkuu Bwana James Hogan amesema: “Rubani wetu na wafanyakazi
wa ndege wanapaswa kupongezwa sana kwa utulivu wao na namna ambavyo
walishughulikia tukio hili la aina yake kwa utaalamu mkubwa, na huduma
waliyoionesha kwa abiria japo kuwa wengi wao walikuwa wamejeruhiwa. Ni
ushahidi wa mafunzo ya kiwango cha juu yanayotolewa kwa wafanyakazi wetu
ndio sababu athari za msukosuko ulipunguzwa. Wakati huo hakuna kabisa
usalama wa ndege,abiria au wafanyakazi walioathirika.”
Shirika la ndege la Etihad linashirikiana kikamilifu na Mamlaka za Indonesia katika uchunguzi wao.
MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI WA UMEME WA GESI TOKA JAPAN
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya
Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe
wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo
ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia
kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) .
No comments:
Post a Comment