Akizungumza na waandishi habari leo Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi
wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro amesema
kuwa mtu aliyetambeliwa kiasi cha fedha hizo alilipa kupitia benki ya
CRDB kwa madini bandia ya dhahabu Kilogram 20 zenye thamani ya Dola za
Kimarekani 40,000.
Amesema baada ya mtu huyo kulipa fedha hizo alikabidhiwa vipande
vitatu vya madini venye uzito wa Kilogram 212 na kugundua kuwa ni madini
bandia.
Jeshi la polisi lilipompekuwa ofisini kwake na nyumbani kwake
walimkuta ,Chuma cha kuchomea madini,Mashine ya kupima madini ,vifaa vya
kubania (Seal 53) pamoja na taarifa mbalimbali za malipo ambayo ameweka
benki na kutoa.
Mtui ambaye anadaiwa kuwa ni tapeli wa madini pandia anamiliki kampuni ya Crown Logistics and Cargo Handling Limiited.
Wakati huo huo jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam
linamskilia Waziri Jamal (39) mkazi wa Mbezi Msakuzi ambaye wamemkamata
na silaha moja aina ya Bastola Browning 6.35 Calbre yenye namba za
usajili A.08416/ Car 90522 na baada ya kumhoji wameweza kubaini mtandao
wao wa watu nane.
Aidha jeshi la polisi limesema kuwa askari aliyeuawa jana kwa kupigwa
risasi ni wa mkoa wa pwani na kuahidi lazima watakamatwa wote
waliohusika.
=============================================
No comments:
Post a Comment