Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Picha Maktaba)
Na EmanuelMadafa,Mbeya(Jamiimojablogu)
SERIKALI Mkoani Mbeya imeagiza kufutwa kwa hati ya kiwanja
kilichotolewa na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye chanzo kikuu cha
maji kilichopo eneo la Nyibuko kata ya Mwakibete kwa matumizi ya makazi.
Agizo hilo, limetolwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya
kutembelea na kukagua chanzo kikuu cha maji cha Nzovwe, chenye uwezo wa
kuzalisha mita 12 za ujazo kwa siku na kusambaza maji kwa asilimia 41
kwa wakazi wa jiji la Mbeya wapatao zaidi ya 200,000.
Kiwanja hicho ambacho kipo karibu na eneo la chanzo cha maji cha Nzovwe,
kilitolewa na maafisa ardhi, idara ya mipango miji kwa ajili ya
matumizi ya makazi na kumilikiwa na mtu binafsi aliyetajwa kwa jina moja
la Mwakasala.
Makala amesema, chanzo hicho cha maji ndio tegemezi kwa kusambaza huduma
ya maji kwa wananchi wa Jiji la Mbeya, hivyo kama kitaachwa na
kuharibiwa, wananchi zaidi ya 200,000 wapo hatarini kuikosa huduma hiyo
ambayo ni haki yao ya msingi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali iliwaondoa wananchi wote waliokuwa
wanaishi au kuendesha shughuli zao za kiuchumi ndani ya mita 60 na
kuwalipa fidia zao hivyo hatua ya wananchi hao kuendelea kuishia mahali
hapo ni kukaidi agizo la serikali.
Amebainisha kuwa kiwango kikubwa cha upotevu wa maji kwa asilimia 31
inatokana na baadhi ya vyanzo vya maji kuharibiwa kwa kufanyika kwa
shughuli za kibinadamu, kulisha mifugo au kujenga nyumba za makazi
pamoja na mabadiliko ya kihaidrolojia.
Hata hivyo, Mkuu huyo aliutaka uongozi wa mamlaka ya maji kwa
kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuhakikisha
wanalisiamamia zoezi hilo la kumondoa mvamizi huyo ndani ya siku tatu.
“Wananchi wengine wameondoka tena kwa hiari yao wenyewe, sasa kwa nini
huyu atuchezee mchezo mchafu?.. kwa hili sikubaliani nalo, huku
akiwataka wananchi ambao ni vijana kulilinda eneo hilo na kuwaonya wale
ambao watakubali kutumiwa na mtu au watu kufanya fujo,”alisema.
No comments:
Post a Comment