Akiongelea
tukio hilo Fizo amesema kwake ni bahati kubwa sana kupata nafasi hiyo
kwa filamu yake kuwa ya kwanza kutoka kampuni ya Steps Entertainment
kuanza kuonyeshwa katika Jumba la sinema katika Big Screen na kuingia
katika hatua nyingine ya biashara.
“Namshukru
sana Mwenyezimungu kwa kupata bahati hii nimetengeneza filamu kubwa na
inaonyeshwa katika ukumbi wa filamu kwa hadhi kubwa, nipo na wasanii
wakubwa Gabo zigamba na wengine,”anasema Man Fizo.
Filamu
ya Nimekosea wapi? inatarajia kuonyeshwa tarehe 11.May.2016 kwenye
Bongo Movie Premiere kuanzia saa 1:00 ambapo wasanii watapita katika Red
Carpet na kuingia ukumbi kwa ajili ya kuona sinema yenye ubora mkubwa.
“Pia
tunashukru kwa wapenzi wa kazi zetu kusapoti kwa kila hatua kwani
wamekuwa karibu nasi na naamini kuwa katika jambo hili muhimu kwa tasnia
ya filamu watatuunga mkono, kiingilio ni 5,000/ tu za Kitanzania
msikose,”anasema Man Fizo.
Tarehe
12.may.2016 hadi tarehe 15. May. 2016 saa 2:00 kamili usiku kila siku
sinema ya Nimekosea Wapi? itaonyeshwa katika ukumbi wa Suncrest Cineplex
Cinemas na wapenzi wa filamu kujionea hatua kubwa kutoka kwa wasanii wa
kitanzania wakifanya mambo makubwa.
Na
tarehe 16. May. 2016 filamu ya Nimekosea wapi itaingia mtaani kwa maana
hatua ya Dvd. Tanzania inaingia katika hatua nyingine kwa filamu zetu
kuonyeshwa katika kumbi za sinema hatua muhimu sana katika ukuaji wa
tasnia ya filamu Tanzania kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.
Filamu
ya Nimekosea Wapi? inafungua njia kwa kazi za kitanzania kuonyeshwa
katika majumba ya sinema kwa kiingilio cha 5,000/ ikiwa ni njia ya
kuwafanya watu wapende kazi za ndani na itaonyeshwa kwa siku tano
mfululizo.
No comments:
Post a Comment