WATANZANIA WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI SHINDANO LA KUONGEZA KIPATO
“Master Card Foundation inafanya kazi na mashirika yenye maono ili
kuleta zaidi upatikanaji wa elimu, mafunzo ya ujuzi na huduma za
kifedha kwa watu wanaoishi katika umaskini barani Afrika, ikiongozwa na
dira ya kuboresha mafunzo na kuongeza ushirikishwaji wa upatikanaji wa
kifedha ili kupunguza umaskini,” alisema Kivuti.
Kivuti alisema kuwa, kaya nyingi za vijijini barani Afrika
hazishirikishwi katika masuala ya kifedha na zaidi ya asilimia 70 za
familia Kusini mwa Jangwa la Sahara sehemu kubwa ya mapato yao
yanatokana na shughuli za kilimo, wakati huohuo watoa huduma za kifedha
wanakabiliana na changamoto kadhaa katika kuifikia jamii, hivyo Master
Card likaamua kusaidia miradi ambayo ina uwezo wa kuleta mabadiliko
chanya.
MGODI WA DHAHABU WA BULHANHLU WAINGIA MAKUBALIANO NA TAASISI YA BENJAMINI WILLIAM MKAPA YA KUBORESHA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akibadilishana hati za
makubaliano na Afisa Mkuu wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa,Dkt Ellen
Mkondya wakati wa hafla ya makabidhiano ya hati hizo iliyofanyika
wilayani Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Graham Crew pamoja na Afisa Mkuu wa
Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt Ellen Mkondya wakitia saini katika
hati za makubaliano ya kuboresha mradi wa huduma ya afya ,Zoezi la
utiaji saini ulishuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita
Kawawa(kulia) ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala,Patrick Karangwa
(nyuma ya mkuu wa wilaya) pamoja na viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu
,Elias Kasitila na Mganga Mkuu wa wilaya ya Msalala Dkt Hamad Nyembea.
Meneja wa Mgodi wa Bulyanhulu ,Graham Crew akizungumza mara baada ya
kutiliana saini makubaliano ya kuboresha huduma za Afya na Taasisi ya
Benjamini William Mkapa wakati wa hafla iliyofanyika katika mji wa
Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Vita Kawawa akitoa neno la shukrani kwa
uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kwa michango ambao wameendelea
kutoa kwa wilaya ya Kahama na Msalala.
No comments:
Post a Comment