UPDATES: MSIBA WA MTOTO WA ANKAL
Stara
fashion week imedhaminiwa na Maximalipo, Hijab Couture, Hijabi Central
Tz, Kanzu Point, Cordoba School, Speedy Print, I-view Studio, Vayle
Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden Restaurant, Event Lights,
Sofia Production, Clouds Media na wengineo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata
utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF)
lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto)
ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu
na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister
Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza
kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan
Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Phillip Mpango. Picha zote na Mafoto Blog
"Wale
wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi
kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown
yote, atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama
wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa
dhati, wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za
sukari, halafu
unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi
mtukufu wa Ramadhani utakapoingia watu wakose sukari, dawa yao ninayo"
Amesema Rais Magufuli.
Chama
cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama
wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu
Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne
Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa
ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa
marudio wa Zanzibar.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu
wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa
chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid
amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika
mikakati yake ya kuchukua dola.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano
mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza
amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi kinakwenda
kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama
Chochote cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili
wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki
katika chaguzi.
Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe
wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo
Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo
amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa na
Wajasiriamali wadogowadogo kwenye maonesho ya maadhimisho ya siku ya
Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa kwanza
Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa
yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini
Dodoma.
Baadhi ya Wajasiriamali wadogowadogo wakifuatilia maonesho ya
maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa
Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na
Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya
Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akimkabidhi cheti mmoja kati waliofanya vizuri kwenye maonesho
ya maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa
Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke. Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na
Jumuiya ya UWT Taifa yamefanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya
Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akionesha Tunzo alizokabidhiwa na UWT Taifa kwa ajili ya
kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa Kwanza Mwanamke kwenye
maadhimisho ya siku ya Mama yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa
yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini
Dodoma.
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,alipokua akihutubia kwenye
maadhimisho ya siku ya Mama na sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa
Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika
viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akihutubia Wanawake kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na
sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais Mwanamke wa kwanza
yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo Mei 8,2016
katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Vikundi mbalimbali vya Ngoma Vikitumbuiza kwenye maadhimisho ya siku ya
Mama na kumpongeza Makamu wa Rais kwa kuchaguliwa Makamu wa Rais wa
kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa yaliyofanyika leo
Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akiagana na Wanawake na Wananchi wa Dodoma baada ya kuwahutubia
kwenye maadhimisho ya siku ya Mama na kumpongeza kwa kuchaguliwa Makamu
wa Rais wa kwanza Mwanamke yaliyoandaliwa na Jumuiya ya UWT Taifa
yaliyofanyika leo Mei 8,2016 katika viwanja vya Nyerere Square mjini
Dodoma.(Picha na OMR)
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi
Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel,
kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika hafla ya uzinduzi
wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es
Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce
Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
No comments:
Post a Comment