Habarini za muda na wakati kama huu
wapendwa watanzania wenzangu. Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vizuri katika
shughuli zenu za kila siku.
Nichukue fursa hii kuwashukuru Mtandao wa
wanafunzi TSNP na vyombo vya habari nchini kwa kukubali kushirikiana nami
GIBSON JOHNSON (Spika wa Bunge chuo cha elimu UDOM) na wanafunzi wa SPECIAL
DIPLOMA KWA UJUMLA katika kutafuta na kutetea maslahi yao juu ya kile
kinachoitwa uonevu waliotendewa na serikali. Lakini pia niwashukuru wanasiasa
na wanaharakati mbalimbali waliopaza sauti zao kukemea vikali ukiukwaji wa utu
kwa wanafunzi wa special diploma UDOM.
Nimepitia vizuri maelezo ya serikali juu
ya msimamo wake na hatma katika suala hili la UDOM lakini nimegundua pia haki
haijafuatwa hata kidogo zaidi sana ubabe ndio uliotumika katika maamuzi haya.
Nasema hivyo kwasababu zifuatazo;
1. Vigezo vilivyotumika katika kuchambua
wenye sifa na wasio na sifa si vile vilivyotumika mwanzo wakati wanafunzi hawa
wanachaguliwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais mstaafu na waziri
Mkuu pamoja na waziri wa elimu. Tamko la sasa la serikali linasema kuwa
wanatakiwa wenye angalau krediti mbili kwenye tahasusi (comb) hii ni kinyume na
makubaliano ya awali ambayo yalikuwa yakihitaji mtu awe na angalau C moja
kwenye tahasusi (comb) atakayosoma.
Serikali imetoa msimamo wake ambao ni
hasi kwa wanafunzi 1210 waliokuwa wanasoma diploma in primary kwani imesema
walikuwa nje ya malengo hivyo mpango huu wa diploma maalumu ulikuwa hauwahusu
bali ulikuwa maalumu kwa wale wa sekondari. Jambo hili ni kinyume na haki
kabisa kwani wamepotezewa muda mwingi sana kwani kuna waliokuwa wanasoma mwaka
wa kwanza na wengine mwaka wa pili ambao wote walichaguliwa na mamlaka husika
yaani TCU pamoja na NACTE na hawakujichagua wenyewe. Hivyo basi kulingana na
hivyo seeikali haina budi kuwatafutia vyuo ambavyo watamalizia masomo yao
kinyume na kuwaacha tu kwa kuwaambia haiwatambui, huu ni uzalilishaji mkubwa na
ukiukwaji wa haki.
My Note:
Ni vizuri sana kuihimiza serikali kufuata
sheria, kanuni na taratibu katika kuiongoza nchi na si kuongozwa na mawazo ya
mtu mmoja tu. Pili, suala la kuwaacha nyumbani wanafunzi waliokuwa wanasoma
diploma in primary kwa kigezo eti haikuwatambua halileti tija wala mantiki
yoyote kwa taifa na wananchi pia hivyo serikali inapaswa kuliangalia upya jambo
hili na kuwawajibisha wahusika waliokubali kuwepo kwa na sio program hii.
Mwisho:
Niwaombe vijana wote waliokumbwa na janga
hili tuwe na ushirikiano na umoja wa hali ya juu katika kuitafuta haki.
Imetolewa na;
Gibson Johnson E.
No comments:
Post a Comment