============================================
Serikali yapongezwa kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum
Na: Frank Shija, MAELEZO
Msichana anayetumia Ulimi katika kuandika miswada ya Filamu amewashukuru wadau mbambali kwa misaada yao iliyomfanikisha kuweza kushiriki katika mashindano ya uandishi wa miswada ya Filamu yaliyofanyika mjini Zanzibar.
Shukuruani hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuhusu malengo yake ya kuanzisha Taasisi itakayosaidia watu wenye matatizo kama yake.
Wakonta amesema kuwa kwa namna ya kipekee kabisa anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia kwa Bodi ya Filamu kumgharamia nauli iliyomsaidia kutoka kijijini kwa Kipili wilayani Nkasi mkaani Rukwa hadi kuanikisha ushiriki wake katika mashindano hayo.
“Ninaishukuru sana kwa kipekeke Serikali ya awamu ya Tano, kwani kupitia kwa KatIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu nimeweza kusaidiwa fedha iliyoniwezesha kushiriki katika mashindano ya Uandishi wa Miswada ya Filamu nashukuru sana”. Alisema Wakonta.
Aliongeza kuwa pamoja na Serikali kumpa msaada huo wapo baadhi ya wadau ambao nao wametoa michango yao katika kufanikisha Kampeni yake ambapo amewataja wadau hao kuwa ni Clouds Media waliomsaidia kuhabarisha umma, Joyce Kiria aliye safiri hadi kijijini kwao Kipili ili kumsaidia kupitia kipindi chake cha Wanawake Live.
Wengine ni pamoja na magazeti ya Mwananchi na Uwazi kupitia waliokuwa msaada kupitia habari zao, Fastjet waliomsaidia huduma ya usafiri kutoka Mbeya na Hoteli ya Serena waliomsaidia upande wa malazi wakati alipofika Dar es Salaam akitoea kijini kwao Kipili, Mkoani Rukwa.
Ametoa rai kwa wadau wenye nafasi zao kujitokeza na kushirikina naye katika kukuza kipaji chake ili aweze kukitumia katika kuleta tija kwa Taifa kwani kupitia Filamu unaweza kutangaza Utalii wanchi na ata biashara.
Wakonta alikuwa miongoni mwa washiriki 15 kutoka Afrika Mashariki katika Shindano la Uandishi wa Miswada ya Filamu la Maisha Scree Writer’s Laboratory Course lililofanyika mjini Zanzibar na huku yeye akiwa mshiriki pekee anayetumia Ulimi katika kuandika.
=============================================
No comments:
Post a Comment