TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, July 21, 2016
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria akutana na LHRC na kuzungumza nao
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amekutana na Ujumbe wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC ) ulioongozwa na dkt Hellen Kijo Bisimba kikao hicho kilikuwa na lengo la kubadilishana mawazo juu ya sekta ya sheria na kuangalia upatikanaji wa haki kwa wananchi wote na ulinzi wa haki za binadamu nchini.
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Wizarani mhe. Waziri alikipongeza kituo cha LHRC kwa kazi nzuri inayofanya hasa ya kuwapatia msaada wa kisheria wananchi wenye uhitaji na kuwahakikishia kuwa Serikali iko mbioni kutunga Sheria itakayowaongoza na kuwasimamia watoa msaada wa kisheria sheria ambayo itawatambua wasaidizi wa sheria nchini
Ujumbe huo ulitaka kujua maendeleo ya masuala ya upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania, marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo walisema zinakandamiza haki za binadamu na utungwaji wa sheria mpya nchini.
Ujumbe huo pia uliongelea utendaji wa Mahakama katika maeneo ya gharama za ufunguaji kesi ziko juu hali ambayo inawafanya wananchi wengi kushindwa kuzimudu gharama hizo, kurundikana kwa kesi na upoteaji wa majalada na kupongeza uamuzi wa kuanzisha Mahakama maalum ya kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi na uongezaji wa majaji ili kuendana na wingi wa kesi nchini ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa mahakama hiyo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment