TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, July 17, 2016

MASHINDANO YA KOMBE LA RPC LINDI CUP 2016 YAZIDI KUSHIKA KASI HUKU ZAWADI ZIKIZIDI KUTAWALA UWANJANI KILA SIKU


Michuano ya Kombe la R.P C Cup LINDI 2016 , limezidi kushika kasi baada ya timu mbali mbali kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Michuano hiyo imeanza bila Uzinduzi kutokana na Ujio wa Waziri Mkuu kuingilia kati Ratiba ya Ligi hiyo na hivyo kufanya michuano kuanza bila Shamrashamra za Uzinduzi hadi Waziri Mkuu atakapokuwa ameondoka ili kuwapa Nafasi na Maafisa wa Serikali kuweza kuhudhuria kwenye Uzinduzi akiwemo Mwenye Mashindano yake ambaye ni R.P.C Mkoa wa Lindi, Afande Renatha Mzinga.

Waratibu na Wasimamizi wa Michuano Hiyo Afande Msafiri ambaye ni Afisa katika Jeshi la Polisi, na Mpalule Shaaban ambaye ni Mkurugenzi wa Mashujaa Radio Lindi,ambao kwa pamoja ndiyo waandaaji wa michuano hiyo, wameendelea kuyaendesha Mashindano hayo kwa hali ya juu ikiwemo kusimamia utulivu wa Uwanja, pamoja na kuhakikisha sheria zote za mchezo wa mpira wa miguu zikisimamiwa vizuri.

Jumla ya Timu 18 zinashiriki Michuano hiyo ambapo mpaka michezo hiyo inamalizika kutakuwa na Idadi ya Michezo 75 na mzunguko wa kwanza unatarajiwa kukamilika leo baada ya timu zote 18 kucheza michezo yake ya awali huku kukiwa na zawadi mbali mbali uwanjani kwa ajili ya makocha na timu zinazoibuka kidedea.

Aidha zawadi za Vikombe kwa washindi watatu wa kwanza, samnamba na medali zitatolewa pamoja na Zawadi zingine kwa mfungaji bora na mchezaji bora kiatu cha Dhahabu, Kipa Bora dhahabu ya Grovu yenye alama ya Kipa, Timu yenye Nidhamu Kikombe, Kikundi bora cha Ushangiliaji Kikombe, Mchezaji Bora Chipukizi Kiatu cha Dhahabu.

Zawadi zingine ni kwa Makocha ambao wanapata Filimbi za Kisasa wanazoendelea kupewa na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania pamoja na Stop Watch na wanakabidhiwa wakati wa Michezo pamoja na Furana zilizotolewa na Kampuni ya T-Mark Tanzania pamoja na Furana za GSM kwa ajili ya Waamuzi na Vikundi vya Uhamasishaji.

Kilele cha Michuano hiyo ni tarehe 25 ya mwezi wa nane ambayo itakuwa siku ya kilele cha siku ya Polisi Day.

Mashindano haya yanadhaminiwa na R.P.C Mkoa wa Lindi, Mashujaa Radio, BIG BON, T-MARK TANZANIA, GSM Wauzaji wa PIKIPIKI ZA GSM na Magodoro ya GSM, CxC Tours & Safaris, FOLEN PLAN CLINIC, Miss Demokrasia Tanzania, MPALULEBLOGS: na PIMAK LIMITED.

No comments:

Post a Comment