Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa akiongea na wadau mbalimbali wa uchumi nchini hawapo pichani wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa taasisi binafsi inayojihusisha na biashara Namaingo Business Agency Bi. Biubwa Ibrahim akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Mdau wa Uchumi nchini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima (NIC) Bw. Sam Kamanga akichangia hoja wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
wadau mbalimbali wa uchumi nchini wakifuatilia kwa makini majadiliano ya wachngiaji mada wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji uliofayika jijini Dar es salaam.
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali imesisitiza matumizi ya bidhaa za ndani ya nchi zinazotengenezwa na watanzania ili kukuza uchumi wa nchi na kupanua ukubwa wa masoko ili kuleta maendeleo.
Akizungumza hayo wakati wa kufunga mkutano wa mwaka wa mashauriano ya ushiriki wa watanzania Katika uwekezaji Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa amesema kuwa watanzania wajifunze kupenda na kutumia bidhaa za ndani ili kuweza kuinua nchi kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa letu.
“Ni lazima watanzania tujifunze kubadilika kifikra na kimtazamo katika kutumia bidhaa zilizopo nchini kuchangia Katika kukuza uchumi wa nchi yetu ili kupiga hatua Katika maendeleo ya Tanzania”alisisitiza Bw.Uledi.
Aidha Bw. Uledi amesema kuwa mwekezaji yeyote awe wa ndani au wa kigeni anapaswa kutumia wafanyakazi wa nchini kama kama anataka kuwekeza Katika Taifa letu ili kutoa fursa kwa watanzania kushiriki Katika kuinua uchumi.
“Mwekezaji wa kigeni au wa ndani inampasa atumie wataalamu na wafanyakazi wa Tanzania kama anataka kuwekeza nchini mwetu ili vijana wetu wa kitanzania wapate fursa ya kuchangia Katika kuinua uchumi wa nchi”.aliongza Bw. Uledi.
Mbali na hayo Bw. Uledi Mussa amesema kuwa kiwanda chochote kinachowekeza nchini wanapaswa kutumia malighafi kutoka Tanzania ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo Katika Taifa letu kwa ujumla.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa amesema kuwa Katika mkutano huo wenye kauli mbiu ya “Ongeza Ushiriki Inua Uchumi” umetoka na mkakati wa kuhakikisha makampuni yote ya uwekezaji kutoka nje yajiandikishe Katika soko la Hisa (DSE) ili kuongeza ushirikina umiliki wa watanzania Katika makampuni husika.
Aidha bi. Issa ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuwa wakandarasi wote ambao wa ndani wanapewa malipo yao kwa wakati kama walivyokubaliana ili kumsaidia mtanzania kushiriki Katika kukuza uchumi wa nchi.
No comments:
Post a Comment