KUTOA MSAADA HAIMAANISHI NI KUTENGENEZA MAZINGIRA YA KUKWEPA KODI-MAKONDA
.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati)akipokea moja ya bati kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo, Subash Patel ikiwa ni sehemu msaada wa
kupaulia vyumba madarasa leo jijini Dar es Salaa , Kushoto ni Katibu
Tawala wa Mkoa, Thelesia Mmbando.
Amesema kuwa wenye viwanda kuacha kutumia mitaro ya mvua kutiririsha maji na kutengeneza mifumo yao.
=====================================
MKURUGENZI KISHAPU AKUTANA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI,AWATAKA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA NA RASILIMALI ZA SERIKALI.
=============================================
Dk shein azungumza na kamati ya uchangisgaji fedha za madawati
======================================
Rais Magufuli aagiza wafanyakazi wa Polisi ambao ni raia wapelekwe Utumishi
==================================================
Lukuvi amteua Jaji wa Mahakama Kuu kuchunguza mgogoro wa ardhi wa miaka 27
WAZIRI
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amemteua
Jaji Jacob Mwambejele wa Mahakama Kuu-Kitengo cha Biashara kuchunguza
mgogoro wa Kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani vya Mfuru, Mbigiri,
Mandengwa, Dumila, Matongolo na Maboiga vilivyopo Wilayani Kilosa, Mkoa
wa Morogoro ili kupata suluhisho la kudumu la mgogoro ambao umedumu kwa
miaka takribani 27.
=================================================
RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO
Pamoja na kutoa
agizo la kutaka wasio askari polisi kuondolewa katika utumishi wa jeshi la
polisi, Rais Magufuli pia ameagiza jeshi hilo lichukue hatua dhidi ya wote
wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa fedha wakiwemo wanaodaiwa kuiba mabilioni ya
shilingi zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa sare za askari mwaka jana 2015.
"Mnajua
kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta
Jenerali wa Polisi) ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa
ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi
mnae palepale, mnashindwa kumshika.
"Kama
mnafikiri kuwa na raia katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni
raia wote na wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi?
hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni askari
polisi? Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa yanaletwa na
raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu mengine, IGP kaorodheshe
raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili waondolewe na tuwapangie kazi
nyingine uraiani" Amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais
Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayofanya iliyoliwezesha
kujenga imani kubwa kwa watanzania na ametaka viongozi wa Jeshi hilo wawaongoze
askari walio chini yao vizuri, wawatie moyo na waache vitendo vya kuwakatisha
tamaa kwa kuwaadhibu ama kuwatisha pale wanapochukua hatua stahiki dhidi watu
wanaovunja sheria.
"Sasa mimi
niwaombe nyinyi, wale wadogo mnaowaongoza mkawape mamlaka ya kutimiza wajibu
wao, hata kama ameshika gari la IGP liache lishikwe IGP atakwenda kujieleza
mwenyewe, hata akishika gari la RPC afanye hivyohivyo, hata akishika gari la
Waziri au gari la Rais mwacheni atekeleze wajibu wake, sheria ni msumeno,
tunawanyima nguvu hawa wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria
halafu unamwambia liachie, ukifanya hivyo aliyeshikwa anatoka pale akiwa anatamba
kwelikweli na yule askari unamvunja nguvu ya kufanya kazi"
Amesisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia
amelitaka jeshi hilo kuungana na vyombo vingine vya serikali katika kutekeleza
shughuli zake zikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bandarini,
katika sekta ya utalii na maeneo mengine, kukabiliana na vitendo vya rushwa na
kuondoa watumishi hewa.
Tukio hili la
Naibu Makamishna wa Polisi na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kula kiapo
cha uadilifu kwa viongozi wa umma limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji
Mstaafu Salome Kaganda na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.
George Mcheche Masaju, Makatibu Wakuu na Viongozi wa vyombo vya Ulinzi na
Usalama.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
18 Julai,
2016
=====================================================
BLESSING KUFAYA UCHANGIAJI WA VIFAA VYA SHULE KWA WANAFUNZI WASIO NA UWEZO.
=======================================
MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 27 WA AU NCHINI RWANDA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa
Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika ukumbi wa KCC mjini Kigali
Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano
huo.Picha na OMR.
KIGALI, RWANDA.
Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Afrika (AU) kwamba itaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama wa AU katika kujadili changamoto za kiusalama zinazolikabili Bara la Afrika kwa njia ya mazungumzo na upatanishi kama inavyoelekeza Katiba ya umoja huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akichangia mada kuhusu Hali ya amani na usalama katika Bara la Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika hapa Kigali, Rwanda.Mheshimiwa Samia alisema Tanzania inasikitishwa na inalaani vikali matukio ya uvunjifu wa amani yanayoendelea kujitokeza katika baadhi ya nchi za Kiafrika kiasi cha kutishia usalama wa raia.
Alielezea mauaji ya Hafsa Mossi, aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na waziri wa zamani wa Burundi na mapigano ya hivi karibuni Sudan ya Kusini ambapo mamia ya raia wasiokuwa na hatia waliuwawa na wengine maelfu wameachwa bila makazi kwamba ni muendelezo wa uvunjifu wa amani katika nchi hizo.
Aliwataka wadau husika katika nchi za Burundi na Sudan ya Kusini kushiriki kikamilifu katika mazungumzo yanayoendelea kwa kuwa hiyo ndiyo njia muafaka ya kuleta amani, usalama na utulivu wa kudumu katika nchi zao.Aidha, Makamu wa Rais ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo aliiomba Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuisadia Sudan ya Kusini katika kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika mgogoro ulioikumba nchi hiyo.
Akichangia kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Makamu wa Rais alisema Tanzania kwa ujumla inaunga mkono msimamo wa Afrika wa kuwa na viti viwili katika baraza hilo na kura ya turufu bila ya masharti yoyote.Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo viongozi walisisitiza suala la kuimarisha umoja baina ya nchi wanachama na kusema hiyo ndiyo nguzo muhimu katika kukuza uchumi na ustawi wa wananchi wa Bara la Afrika.
Katika mkutano huo kulikuwa na uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya Afrika ambayo ilitolewa kwa Mwenyekiti wa AU, Rais Idris Deby wa Chad na nchi mwenyeji wa mkutano, Rais Paul Kagame wa Rwanda.Mkutano huo ambao ulizungumzia pia gharama za kuendesha umoja huo na masuala ya haki za wanawake ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi zaidi ya 35, Marais wastaafu, wake wa Marais pamoja na viongozi wa serikali.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais

=========================================
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.
VODACOM YAFANIKISHA MAWASILIANO KATIKA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA TIMU YA "TRECK4MANDELA " MANDELA KUTOKA AFRIKA KUSINI
================================================
No comments:
Post a Comment