TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 2, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWASILI MBARALI, AENDELEA NA ZIARA YAKE


Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukizungumza na wananchi baada ya kuwasili katika mji wa Igawa wakati ukielekea Ludewa wilayani Mbarali Kinana amepata nafasi ya kuongea na wananchi wa eneo hilo kama anavyoonekana Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki  Mh. Godfrey Zambi, Leo katibu mkuu huyo anafanya ziara katika wilaya ya Mbarali akikagua miradi ya maendeleo na kuongea na wananchi kuimarisha uhai wa chama cha Mapinduzi, Katika msafara huo Kinana ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC  Itikadi, Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  3 
Jengo la ofisi ya CCM  kata Ihanga iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana leo  5 

KIINGILIO MECHI YA TANZANITE BUKU TU, NENDA KAPATE BURUDANI!!

DSC_0184 
Washabiki watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini watalipa kiingilio cha sh. 1,000.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Kiingilio cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange. Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WAZIRI MKUU MHE. PINDA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA SADC


PG4A7298 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Katibu Mkuu wa SADC, Stergomena Tax Bamwenda, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Desemba  2, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

AJALI YAB MALORI JANA YAGONGANA NA KUZIBA NJIA ENEO LA WAMI,

Malori yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la mto wami
Foleni ni kubwa sana ya mabasi yaendayo mikoa ya Tanga,Arusha Na Kilimanjaro
Ajali mbaya imetokea mda huu eneo la mto wami na kusababisha Foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo,Chanzo cha ajali hiyo inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo.Polisi wanaendelea na jitihada za za kuyatoa ili njia ipatikane kwa ukubwa zaidi ili kuruhusu upitaji mzuri wa magari.

WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA OFISI ZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

IMG_0032 
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo  Pinda akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa  Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura kuhusu  baadhi ya mitambo iliyopo nje ya jengo la Simu (Telephone House). Wa pili kutoka  kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa. IMG_0042 
Afisa Mtendaji wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akitoa taarifa fupi kuhusu  utendaji wa TTCL na jinsi kamuni hiyo  ilivyojidhatiti katika kujenga, kusimamia na kuendesha mkongo wa Taifa wa Mawasilino. IMG_0076 
Afisa Mtendaji wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akimuonesha waziri mkuu mkongo halisi (fibre) wakati wa ziara yake katika kituo maalum cha uangalizi wa mkongo wa Taifa (Network Observation Centre).  IMG_0086 
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo namna mitambo ya mkongo wa taifa inavyofanya kazi  kutoka kwa Mhandisi Adam Mwaipungu wakati wa ziara yake katika ofisi hizo. IMG_0029 
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa( Kushoto) pamoja na msafara wa  Waziri Mkuu wakielekea katika kituo maalumu cha uangalizi wa mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

SAUDI PRINCESS VISIT SERENGETI NATIONAL PARK

1-5 
Saudi Arabian Ambassador to Tanzania H.E. Hani Mominah (black cap) talking to Chief Park Warden of Serengeti National Park Mr. William Mwakilema. Far left is Dr. Robert Fumagwa who is the Head of Tanzania Wildlife Research Institute Centre in Serengeti. 3-4 
Princess Haifa Bint AbdulAzizi al Mogrin admiring a Hyrax at Serengeti Visitors Information  Centre.      6 
Princess Haifa enjoying the trail walks. 8 
A lion heading towards the princess convoy.

TANZANIA NATIONAL PARKS
PRESS RELEASE
SERENGETI TO HOST FORTCOMING SAUDI TANZANIA
YOUTH DIALOGUE FORUM
Princess Haifa Bint AbdulAziz al Mogrin of Saudi Arabia has preferred Serengeti National Park for field experience by the participants attending the forthcoming
youth forum in January next year in Arusha.
Princess Haifa made the remarks after visiting Serengeti National Park and managed to see the abundance of wildlife natural resources. “ It is unbelievable, I
used to read about Serengeti through various literatures but today I am overwhelmed from what I can see here. It is my first time in Africa and particularly in Serengeti and I don’t regret at all in coming here” said Princess Haifa.
She said that although the forum organized jointly by Tanzania National Parks and the Saudi Arabian Government will be done in Arusha, the youths attending
the forum will have to visit Serengeti National Park for three days and have a field experience by visiting various conservation projects in the Serengeti such as the Rhino Management Program; Wild dogs Re introduction Project as well as Lion and Hyena Research Projects.
The forthcoming youth forum on Biodiversity Conservation scheduled for January 17–28 next year in Arusha will be attended by youths from both
Tanzanian and Saudi Government.
While in Tanzania, the delegates will have an opportunity to visit also some of the wildlife institutions in the country such as the College of African Wildlife
Management Mweka; Tanzania Wildlife Research Institute; Ngorongoro Conservation Area and Kilimanjaro National Park.
The Princess who is the coordinator of the forum, said that this forum is taking place for the first time in Africa and Tanzania was chosen to host the forum due to its historical background and commitment in protecting wildlife natural resources supported by the peace and security prevailing in the country.
The main theme of the forum is “Construction and Implementation of the Regulatory Framework for Biodiversity Conservation” and will involve about 50 youths from both Tanzania and Saudi Arabia who will have an opportunity to interact and discuss on the future of biodiversity conservation in the two countries.
The youth forum is an initiative by King Abdullah Bin Abdul Aziz for dialogue among the forums worldwide under the program Saudi International Youth
Dialogue Forums. These forums provide the platform for Saudi youth to interact with their peers from different countries, while adopting their creative initiative and solutions under various themes.
Issued by:
Public Relations Department
Tanzania National Parks
02nd December, 2013

WAFANYAKAZI TBL WASHIRIKI KUPIMA KWA HIARI VIRUSI VYA UKIMWI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Tereza Mbando (katikati), akiwasha mshumaa kuzindua zoezi la kupima virusi vya ukimwi kwa hiari kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani. Kulia ni Meneja Raslimali watu wa kampuni hiyo, Bw. David Mafuru.
Muuguzi Mshauri wa kupima maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Bi. Aulelia Kunambi, akimpima Meneja Raslimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. David Mafuru (kulia), wakati wa zoezi maalumu la kupima Ukimwi kwa hiari kwa wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa baada ya kushiriki katika zoezi la kupima ukimwi kwa hiari, wakati wakiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa baada ya kushiriki katika zoezi la kupima ukimwi kwa hiari, wakati wakiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.
Wasanii wa kundi la THT wakitoa burudani kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, wakati wa zoezi la kupima virusi vya ukimwi kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Dar es Salaam

MEREKEBISHO UWANJA WA SOKOINE MBEYA YAANZA KWA KASI KUBWA,


SAM_0720Na Baraka Mpenja -Dar es salaam
Wamiliki wa uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya wameanza rasmi mchakato wa kufanyia marekebisho uwanja huo kama walivyoagizwa na shirikisho la soka Tanzania TFF.
Meneja wa uwanja huo, Modestus Mbande Mwaluka amesema ndani ya wiki mbili watakuwa wamekamilisha marekebisho na baada ya hapo wataanza kumwagilia maji sehemu ya pichi.
“Jana tumeanza kwa kung`oa magoli, leo tunaanza kushughulikia sehemu ya ndani ya uwanja, magreda yameshaagizwa na lazima yaje ili kuutifua na kupanda nyasi mpya. Kizuri pesa ipo ndugu yangu”. Alisema Mwaluka.
“Kizuri zaidi hiki ni kipindi cha mvua jijini hapa, itasaidia sana ukizingatia uwepo wa maji ya bomba. Nyasi zitakua haraka na kubadili mandhari ya uwanja huu”.
Mwaluka amesema wanataka uwanja huo uwe mzuri na utumike katika michuano ya kimataifa, na kwasasa watarekebisha miundo mbinu yote ikiwemo vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji, vyoo na maeneo mengine muhimu.
IMG-20120915-WA0005
“Ujue tulishasema kutoka mwanzo kuwa, tupo katika mkakati madhubuti wa kuufanya uwanja wetu uwe bora, tulianza na uzio, tumeshaimarisha, sasa tunafuata sehemu ya ndani `Pitch`, tutafuata vyumba vya kubadilishia nguo, halafu vyoo na miondombinu mingine”. Aliongeza mwaluka.
Meneja huyo alisitiza kuwa wapenda michezo jijini Mbeya ambao ni mashabiki wa timu za Mbeya  City na Tanzania Prisons wasiwe na wasiwasi kwani timu zao zitatumia uwanja huo, na kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu januari 25, uwanja utakuwa bora”. Alisema Mwaluka.
Endapo uwanja huo hautarekebishwa kwa haraka, timu mbili za ligi kuu Mbeya City na Tanzania Prisons zipo hatarini kucheza nje ya Mbeya, kitendo ambacho kitawanyima fursa kuzishangilia timu zao kwa wingi.

KAIJAGE: TANZANITE NI MAHINDI MACHANGA YANAYOCHIPUKIA, WASIKATISHWE TAMAA SAFARI YAO!!

DSC_0184
Na Baraka Mpenja - Dar es salaam
Wakati timu ya Taifa ya vijana ya wanawake chini ya miaka 20, maarufu kwa jina la Tanzanite ikijiandaa na Mechi ya kwanza ya raundi ya michuano ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 7 mwaka huu, kocha mkuu wa timu za taifa za wanawake , Tanzanite na Twiga stars, Rogasian Kaijage amewaomba watanzania kuwatia moyo vijana hawa kwani hawajaanza kufanikiwa bado.
Kaijage amesema watanzania wasitegemee mafanikio ya haraka kwa timu hii na wale wasichukulie matokeo ya mwanzo kama mafanikio, bali wanatakiwa kuwapa moyo vijana hawa kwani safari yao ni ndefu mno.
“Watanzania tusiwae na tabia ya kutaka mafanikio ya haraka, hawa vijana bado wanayo safari ndefu, cha msingi watanzania hasa wapenda michezo wawape sapoti kubwa ili kufikia mafanikio”. Alisema Kaijage.
“Vijana hawa ni mahindi machanga ndio yanaanza kuchipua, kile wanachokifanya sio mavuno bali ni ishara kuwa wanatakiwa kuungwa mkono. Hawatakiwi kukatishwa tamaa, waungwe mkono kwani wanatengenezwa kwa ajili ya baadaye”. Aliongeza Kaijage.
Kocha huyo alisema katika soka lazima mipango iwekwe, watu wakubali kuwekeza, hivyo wapende michezo wajitokeza kudhamini timu za wanawake kwani wanao uwezo wa kufika mbali zaidi.
Akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Afrika kusini, Kaijage alisema utakuwa mgumu sana kutokana na ubora wao, lakini kila kitu kinawezekana kutokana na maandalizi ya vijana wake.
“Vijana wanaendelea vizuri sana, ninaposema hivyo namaanisha wana morali ya kushindani ili kupata matokeo mazuri. Hivyo watanzania wajiandae kuwapa sapoti vijana wao”. Alisema Kaijage.
Tanzanite ilifuzu raundi ya pili baada ya kuifunga Msumbiji mabao 15-1 ambapo mechi ya kwanza jijini Dar es salaam waliwalamba 10-0 na mechi ya msumbiji wakaitungua 5-1.

Sunday, December 1, 2013

Wachina wasaidia watoto yatima


Mama_Anna_Mkapa
Kibaha. Mwenyekiti wa mfuko wa fursa sawa kwa wote, Mama Anna Mkapa ametoa wito kwa jamii kushiriki kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili kupata mahitaji yao muhimu kama walivyo wengine.
Mama Mkapa alitoa wito huo jana Mjini Kibaha wakati akipokea msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh7 milioni vilivyotolewa na Umoja wa Wafanyabiashara wa China kwenye kijiji cha kulelea watoto yatima Kibaha.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo, alisema kuna haja ya kila mtu kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu ili waweze kuishi kwenye vizuri kama walivyo watoto wenye wazazi.
“Naomba kila mtu na kila jamii itambue umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, kwani watoto hawa ni wetu sote,” alisema Mama Mkapa.
Mama Mkapa alishukuru umoja huo kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu kwenye kituo hicho.
Naye mwakilishi wa Umoja huo wa wafanyabiashara hao Wachina, Hu- Jianxi alisema kuwa wameguswa kuwasaidia watoto hao kwani wanahitaji kusaidiwa ili nao wajisikie kama jamii za watoto wengine wanaolelewa na wazazi wao.

Kampuni 100 bora zatajwa

4e20Abdallah-Kigoda 
Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amesema kuwa, Serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili wawekezaji wa nje na ndani waweze kutekeleza majukumu yao bila kikwazo.
Dk Kigoda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa kwenye hafla ya kuzitambua Kampuni 100 Bora zinazokua kwa kasi nchini (Top 100 Mid–Sized Companies), ambapo Kampuni ya Kipipa Millers Limited ya jijini Mwanza ilishika nafasi ya kwanza.
Kampuni hizo zilitambuliwa na kupewa tuzo kutokana na shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications (MCL) na KPMG Tanzania na kudhaminiwa na Benki ya NBC pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Dk Kigoda alisema shindano hilo linaimarika kila mwaka na lina nafasi kubwa ya kuimarisha uchumi kwa Kampuni za Afrika Mashariki.
Alisema ili kampuni hizo ziweze kufikia mafanikio, Serikali itajitahidi kuweka mazingira yatakayoziwezesha kufanya shughuli zake vizuri na kufanya uzalishaji kwa gharama nafuu.
Alizitaka kampuni zilizofanikiwa kuingia kwenye kundi la kampuni 100 bora, kujitambua kuwa sasa wao ni washindi na hivyo wajitahidi kufanya shughuli zao kitaalamu zaidi.
“Kwa kiwango hiki mlichofikia sasa ni washindi, mfanye kazi zenu kitaalamu zaidi,”  alisema Dk Kigoda.
Alisema kwa sasa Tanzania imeshuka kwenye nchi zenye viwango vizuri vya kufanya biashara duniani, hali inayofanya baadhi ya wawekezaji kukimbia.
Alieleza suala hilo linaipa Serikali changamoto ya kutengeneza mazingira bora na rafiki ili kuvutia wawekezaji kufanya shughuli zao kwa faida.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Zuhura Muro alisema kwa kushirikiana na KPMG, wanaendesha shindano hilo kwa sababu wanaelewa kuwa hiyo ni njia muhimu ya kuhamasisha kampuni kufanya vizuri.
Alisema kuwa, kampuni hizo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na ustawi wake kwani kodi wanazolipa ndizo zinazotumika kwa maendeleo ya nchi.
“Sasa ni wakati wetu wa kuinuka, lakini hatuwezi kuinuka bila kuwa na watu muhimu kama ninyi (kampuni 100 bora) kwani ndiyo mnaotengeneza ajira, nyie ni watu muhimu sana kwa uchumi wa nchi hii,” alisema Muro.
Huu ni mwaka wa tatu wa shindano hilo, mwaka 2011 Kampuni ya BQ Contractors ya Dar es Salaam ilishika nafasi ya kwanza, huku mwaka 2012 Kampuni ya Helvetic Solar Contractors ya jijini Arusha ikichukua nafasi hiyo.
Mara baada ya kutangaza kuwa mshindi jana,  Mkurugenzi Mkuu wa Kipipa Millers Limited, Oliver Matemu alisema hakutarajia kushika nafasi hiyo.
“Nilipokuwa hapo ndani nilikuwa nasikia tu wakitangaza, walipofika nafasi ya 50 bila kusikia tukiitwa nilijua kuwa sisi tumerukwa,” alisema Matemu.
Matemu alisema kuwa, kampuni yake inajishughulisha na usagaji wa nafaka na kuzisambaza pamoja na kusambaza bidhaa za Kiwanda cha Bia cha Tanzania (TBL).
“Kilichotufanya tukaibuka washindi ni namna ambavyo tunajitahidi kuandaa hesabu zetu,” alisema Matemu.
Alisema kuwa, alianza shughuli hiyo kwa kununua unga kwenye mashine za watu na kuusambaza wakati huo akiwa na mtaji wa kati ya Sh1.5 milioni.
“Kwa sasa kwa mwaka nafanya biashara ya kama Sh5 bilioni,” alisema.
Kampuni nyingine zilizoingia kwenye 10 bora ni Otonde Group of Companies Tanzania Limited, iliyoshika nafasi ya pili, SEEDCO Tanzania Limited ya tatu, Kays Logistics Company Limited ya nne, Sihebs Technologies Company Limited  ya tano na Techno Brain Tanzania Limited ya sita. 
Kampuni nyingine ni Anjari Soda Factory Limited nafasi ya saba, NPK Technologies Limited nane, Palray limited ya tisa na Fomcom International Limited  nafasi ya 10.

Wawekezaji wa nyumba waunda umoja

59f0National-Housing-Corporation-NHC
Dar es Salaam. Wawekezaji wa Sekta ya miliki ya nyumba, wameunda umoja wao kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).
Akitoa ufafanuzi kuhusu hatua ya kuanzisha umoja huo uliopewa jina la Chama cha Waendelezaji Miliki Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba, (NHC), Nehemia Mchechu alisema kuwa huo ni mwanzo wa safari ya kuwa na muungano wa wawekezaji katika sekta hiyo wakishirikiana na Serikali.
Mchechu alisema wameanza na wawekezaji wakubwa 30, ambapo kadri siku zinavyokwenda anayetaka kujiunga atafanya hivyo.
Alisema umuhimu wa kuwa na muungano huo ni kuweza kuishauri Serikali kujenga kwa viwango badala ilivyo sasa kila mmoja anafanya kivyake.
Aidha, Mchechu alisema kuwa Tanzania wamechelewa kuanzisha umoja huo kwani mataifa mengi yameshafanya hivyo na kuzitolea mfano nchi za  Kenya, Uganda, Afrika ya Kusini na baadhi ya nchi Ulaya.
“Kwa umoja huu tutajenga imani kwa wateja wetu, ambao watakuwa na sehemu ya kukimbilia wanapoona mambo yanakwenda kinyume na matarajio,” alisema Mchechu.
Naye Mohamed Sharifu, Mtanzania anayeishi Dubai alisema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa itapunguza idadi ya majengo mabovu.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00260
WILAYA YA MOMBA – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 01/12/2013 MAJIRA SAA 01:00HRS HUKO MAENEO YA SIKANYIKA KATA YA TUNDUMA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA MOJA LA SIMBEE S/O ?, ANAYEKADIRIWA NA KUWA NA MIAKA 46-50, MKAZI WA MAPOROMOKO ALIUAWA  NA MWENZAKE MENSON S/O MWAZEMBE, MIAKA 58, MNYIHA NA MKAZI WA MAPOROMOKO, KUJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA ZAHANATI YA TUNDUMA KWA MATIBABU BAADA YA  KUPIGA MARUNGU/FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA  MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILYOTUMIKA NI KUWAVAMIA WAKIWA LINDONI NA KUWAFUNGA KAMBA KISHA KUWASHAMBULIA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA  WITO/RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO WATUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE WENYEWE.

WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO
.
MNAMO TAREHE 30/11/2013 MAJIRA YA SAA 19:00 HRS HUKO KATUMBA  KATA YA  KATUMBA TARAFA YA  TUKUYU WILAYA YA  RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI LISILOFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI WALA DEREVA AINA NA FUSO LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUUU AITWAYE YESAYA S/O MWENDESI, MIAKA 56, MNYAKYUSA, MKAZI WA KATUMBA NA KUSAFARIKI AKIWA ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA TUKUYU. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA DEREVA ALIIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.  KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI HASWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2013 ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAIA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA HUYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA
WILAYA YA KYELA – AJALI YA GARI KUGONGA MTI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 30/11/2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KIJIJI CHA BUGESI KATA YA   KAJUNYUMELE TARAFA YA  UNYAKYUSA WILAYA YA  MKOA WA MBEYA, GARI NO T.896 BBG AINA YA  COROLA LIKIENDESHWA NA DEREVA ANTONY S/O MALILI, MIAKA 31, MNYAKYUSA, MKAZI WA KAJUNYUMELE LILIGONGA MTI NA KUSABABISHA KIFO CHA VICTORIA D/O MALILI, MIAKA 49, MNYAKYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA KAJUNYUMELE NA MAJEREHA KWA ABIRIA MMOJA PAMOJA NA DEREVA. MAJERUHI WAMELAZWA KATIKA HOPITALI YA WILAYA YA  KYELA NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HASPITALINI HAPO, CHANZO CHA AJALI NI  MWENDO KASI. KAIMUKAMANDA WA P OLISI MKOA WAMBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI BORA YA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI HASWA WAKATI HUU KUNAPOELEKEA KUUKARIBISHA 2014 NA KUAGA MWAKA 2013. TUSISHABIKIE MWENDO KASI KWANI AJALI NI NOMA.
 [B.N.MASAKI  – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Msama atoa msaada wa zaidi ya milioni 4!!

Na Mussa Mkama

MKURUGENZI Mtendaji wa Msama Promitions Alex Msama amekabidhi msaada wa magodoro yenye dhamani ya zaidi ya Shilingi milioni 4 kwa kituo cha watoto yatima Luhila Pachane kilichopo Songea Mkoani Ruvuma.
DSC_8730
            Alex Msama
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya ofisi za Msama Promotions Kinondoni Jijini Dar es Salaam jana Msama alisema msaada huo umetoka kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas ambalo linatarajiwa kuanza Desemba 25 jijini hapa na mikoa mingine.
Tamasha hilo la Krismas linatarajia kufanyika katika mikoa mitano, ambapo ni Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Arusha na Dodoma.
Msama alisema kuwa kutokana na maombi ya kituo hicho na kuguswa na hali waliyokuwa nayo ya yatima hao kulala katika mkeka, aliamua kunyofoa sehemu ya fedha zilizokuwa kwenye mfuko wa Tamasha la Krismas na kuamuo kuwasaidi watoto hao ili nao waweze kujisikia wapo katika jamii ya Watanzania.
“Nimeamua kufanya hivyo kutokana na kuguswa na hali halisi waliyonayo yatima hao wa kituo cha Luhila Pachane huko mkoani Ruvuma nikaamua kunyofoa fedha katika mfuko wa Tamasha la Krismas kwa ajili ya kuwasaidi ili nao wajisikie wako pamoja na Watanzania wenzao” alisema Msama na kuongeza kuwa;
“Msaada huo wa magodoro hayo ni zaidi ya shilingi milioni 4, hivyo ninaimani kubwa sasa kwa msaada huu yatima wataniombea kwa Mungu ili Tamasha la Krismas liwe la mafanikio kwani lengo la tamasha hilo ni kuweza kujenga kituo cha kisasa cha watoto yatima na wasiojiweza kwani kiwanja tumeshakiona kipo pale maeneo ya barabara ya Pugu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Mlezi wa kituo hicho ambaye pia ni Katibu wa Bakwata mkoa wa Ruvuma Shekh Abdushakur Omary alisema anamshukuru Msama kwa wema wake aliouonyesha wa kusaidia jamii ya Watanzania wote bila kubagua dini, kabila wala rangi.
“Msama ni mtu wa aina yake hana ubaguzi anashughulikia maombi ya Watanzania wote bila kuangalia dini, kabila, rangi wala utaifa wake kwani amaamini kuwa wote ni wamoja, hivyo naomba nizidi kumuombea aendelee kuwa na moyo huo wa kujitolea kwa ajili ya watu wa taifa lake wasiyojiweza” alisema Omary.
Hata hivyo aliomba Wizara husika kuharakisha upatikanaji wa hati ya kiwanja kile kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kutolea misaada (Center)  pamoja na kiwanda cha kisasa cha kuzalishia kazi za wasanii  kwa manufaa ya Taifa na watu wake, kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia Watanzania wengi wenye ndoto ya kuwa wasanii wakubwa nchini.
“Uwepo wa Msama katika ulimwengu huu kunamuwakilisha Mwenye Mungu, kwani Mungu si mbaguzi kwa watu wake anawapenda wote na anatoa sawa kwa kila mtu, hivyo ndivyo alivyo Msama, kwa moyo mmoja namuombea yeye na taasisi yake isiyokuwa na ubaguzi wa dini kuendelea kuwa hivyo wakati wote” alisema Omari na kuongeza kuwa;
“Naomba Wizara au Waziri husika kuona umuhimu wa ujenzi wa kituo hicho cha kisasa cha kutolea misaada pamoja na kiwanda cha kuzalishia kazi za wasanii, kwani wapo Watanzania wengi wenye vipaji lakini hushindwa kufanya kazi za kisanii kutokana na viwanda kuwa na gharama kubwa wasizoweza kuzimudu”

MZEE NA ‘JAHAZI LAKE’ WACHENGUA MASHABIKI DAR LIVE!!

 
Shabiki aliyevaa kihasara akinengua jukwaani.
 
Khadija Yusuf akiimba.
 
Mzee Yusuf akinengua na mpiga gitaa wake.
…Akiwaimbisha mashabiki.
 
Shabiki akijimwaya.
 
 Kijana aliyetuhumiwa kukwapua pochi akiwa chini ya ulinzi na pochi alilokwapua.
UKUMBI wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam, jana usiku ulifurika mashabiki katika onyesho la bendi ya taarabu ya Jahazi inayoongozwa na staa Mzee Yusuf.

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MNAZI -MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHEREHESHA-DAR ES SALAAM LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwai, chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Angela Ramadhan, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho. Picha na OMR 2-3  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifurahi na mtoto Samir Isagetee (miezi 7) akiwa na Mama yake, Lilian Amani, wakati  alipotembelea katika Banda la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA, katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto waliozaliwa na wazazi wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na yeye kuzaliwa salama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda katika maadhimisho hayo. 5-2 6 
Baadhi ya wanafunzi wakipita na mabango yenye ujumbe mbalimbali mbele ya  Jukwaa Kuu, wakati Makamu alipokuwa akipokea maandamano hayo kwenye  maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es  Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa 3 wa Kitaifa wa Kudhibiti Ukimwi (NMSF3), wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid, (wa pili kulia) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwantum Mahiza, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania, Dkt. Fatma Mrisho.  11 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.  Picha Zote na OMR

KUMEKUCHA - MPINGA CUP WILAYA YA TEMEKE

100_1268 
Timu za kobili na uaminifu zikiwa tayari kwa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mechi, na ukaguzi wa timu hizi ulifanywa na Mratibu wa mashindano haya ya Mpinga cup Mkaguzi msaidizi wa Polisi Agatha Mashayo. 100_1272 
Mratibu wa mashindano haya ya Mpinga cup Mkaguzi msaidizi wa Polisi Agatha Mashayo akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kobil ya Mbagala. 100_1273 
100_1275
Mratibu wa mashindano haya ya Mpinga cup Mkaguzi msaidizi wa Polisi Agatha Mashayo akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Uaminifu ya Mbagala kabla ya mechi kuanza.  
Mchezaji wa timu ya Uaminifu akiwa anamiliki mpira na kujaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya Kobili katika mechi iliyochezwa tarehe 01/12/2013 katika kiwanja cha Mpira za Zakhem Mbagala. 100_1278 
Mratibu wa mashindano haya ya Mpinga cup Mkaguzi msaidizi wa Polisi Agatha Mashayo akikabidhi mpira kama zawadi kwa washindi wa mchezo kati ya timu ya kobil na Uaminifu wakati timu ya Kobili imeibuka na ushindi wa goli 5 – 0.