TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, January 6, 2015

WAENDESHA BODABODA WAJINAFASI KWA MIPASHO DAR LIVE

Khadija Kopa akijipinda kimadaha wakati akifanya ‘mavituz’ stejini.
Kundi la Ogopa Kopa kazini.
Mtoto wa Khadija Kopa aitwae Mohammed Kopa akikamua huku nyuma yake akisapotiwa na wenzake.
Mkali wa miondoko ya Kigodoro, Msaga Sumu, akivamia jukwaa na kuwainua mashabiki waliokaa vitini.
Mashabiki wakijimwaya na burudani ya Kigodoro kutoka kwa Msaga Sumu ambaye alikuwa akisapotiwa na Ogopa Kopa.
Msaga Sumu akimpelekesha Khanifa Khalid anayeserebuka kwa staili ya gwaride.
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa (kulia) na Khanifa Khalid wakikamua.
Aziza Kimodo akikamua.
Shadya Chotara naye akionesha makali yake.
Mashabiki wakifurahia burudani.
WAENDESHA  bodaboda na wamiliki wake walijimwaya na bonge la burudani kutoka kwa Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa na kundi lake la Ogopa Kopa Modern Taarab sambamba na mkali wa muziki wa Kigodoro, Msaga Sumu, kwenye tamasha lao lililofanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhiem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
(PICHA : RICHARD BUKOS/GPL)

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE NDANI YA HARAKATI ZA MAPINDUZI : AKERWA NA WABUNGE MAPAMBO

unnamed
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Bagamoyo mkoani Pwani ,Ridhiwani Kikwete amesema hakugombea nafasi ya ubunge ili kuwa sehemu ya mapambio  bali aliitaka nafasi hiyo ili kuwa sehemu ya suluhisho katika kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Chalinze.
Alisema kiongozi aliyeomba ridhaa ya uongozi kwa wananchi anapaswa kutimiza ahadi alizozitoa na kutatua yale ambayo yapo ndani ya uwezo wake .
Aliyasema hayo juzi,katika kijiji cha Changalikwa na Ng’andi kata ya Mbwewe,Bagamoyo wakati akiendelea na ziara yake ya siku kumi anayoifanya kutembelea kata mbalimbali jimboni hapo kujua kero za wananchi na kueleza yale aliyoyatekeleza na kuyachukulia hatua pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuichagua CCM katika chaguzi zilizopita za sekali ya mitaa,vitongoji na vijiji.
Ridhiwani alisema hayo baada ya kutolewa malalamiko hususan ya maji na kiafya yanayowakabili kwa kiasi kikubwa wakazi wa kijiji cha Ng’andi na Changalikwa.
Wakazi hao walisema wanakabiliwa na tatizo la maji ambalo linawasababishia kutumia maji ya kwenye mabwawa ambayo hayana usalama katika afaya za watu na kufuata maji umbali wa km zaidi ya 5 huku wakinunua dumu la maji kwa kiasi cha sh.500 hadi 700.
Kufuatia kero hizo Ridhiwani alieleza kuwa hatotaka kuona anakuwa sehemu ya pambio katika uongozi wake lakini atahakikisha anatatua kero  kwa wananchi na kushirikiana nao kwa pamoja kwa lengo la kupata suluhisho la kero hizo.
Ridhiwani alisema kwasasa anafanya taratibu ya kumpeleka waziri wa maji ili aweze kwenda kutembelea maeneo yenye kero kubwa ya maji katika kata ya Mbwewe hadi kata ya Kibindu, kujionea hali halisi ya uchungu wanaoupata wananchi.
Alieleza taarifa alishazifikisha kwa waziri husika na anaamini atafika katika maeneo hayo ili aende kujua ukubwa wa tatizo hilo hatimae kulipatia ufumbuzi na kuwaondolea changamoto hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inawapa usumbufu wakinamama  ambao wanatembea umbali mrefu kufuata maji.
“Nataka kusema kwa undani kwa nguvu tunayokwenda nayo na nyie wananchi kutafutia ufumbuzi matatizo mbalimbali mnayoyapata,naamini waziri atakuja  na atatusaidia kero hiyo “alisema Ridhiwani.
Ridhiwani alisema atahakikisha kuyatekeleza yaliyo ndani ya uwezo wake aliyoyaahidi katika muda mfupi wa uongozi wake ,na aliwaomba wananchi kumkumbusha pale anaposahau na kushirikiana nae ili waweze kupiga hatua ya kimaendeleo.
Alisema tayari alishakaa na viongozi wa mamlaka ya maji na kuzungumza nao  ambapo waliahidi kupatiwa maji kwa kujengewa vioski vitatu vya maji ambapo kimoja kitakuwa katika eneo la shule Changalikwa na viwili vitakuwa vijijini  na kukamilisha tanki kubwa la maji lililopo Mbwewe  ili kupeleka maji maeneo mbalimbali.
Aidha alisema serikali bado inaendelea na hatua za kutatua kero hiyo ambapo inachukua hatua ikiwemo kufanya upembuzi yakinifu na  kuendelea na awamu ya tatu ya mradi wa maji wa WAMI ambao utasaidia kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Akizungumzia suala la tatizo la kiafya matika maeneo ya Kibindu na Mbwewe Ridhiwani alieleza kuwa anaendelea kuzungumza na idara husika kuangalia namna ya kujazia watumishi wa afya katika maeneo yenye upungufu mkubwa na kupanga mikakati ya kujenga zahanati katika maeneo ambayo yana ukosefu wa huduma hiyo ili kuwaondolea adha  wananchi wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za kiafya.
Ridhiwani hadi sasa alishatembela kata 3 za Kibindu,Mbwewe na Ubena kwa kutembelea vijiji vinne kwa siku katika kila kata.

Sunday, January 4, 2015

MISS SINGIDA 2014 DORICE MOLLEL ATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA WODI YA WATOTO NJITI

DSC03176Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.
Na Nathaniel Limu, Singida
JUMLA ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa (njiti).
Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.
Hayo yamesemwa na kaimu mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida,Dk.Daniel Tarimo,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba vitakavyotumika kwenye wodi ya watoto njiti katika hospitali ya mkoa mjini hapa.
Kuhusu watoto hao njiti wanaofariki dunia,Dk.Tarimo alisema vifo vingi vinachangiwa na baadhi ya akina mama wajawazito kujifungulia nyumbani mahali hakuna wataalamu wa huduma ya afya.
“Watoto wa aina hii kwa kawaida wanakuwa na matatizo ya kupumua.Sasa mama akijifungulia nyumbani,wakiwa njiani kukimbiza watoto/mtoto wa aina hiyo hospitalini,mtoto/watoto husika hupata tatizo la kupumua linalopelekea vifo vyao”,alifafanua zaidi Dk.Tarimo.
DSC03187Miss Singida 2014 Dorice Mollel akimkabidhi Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, msaada wa vifaa mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwa wodi ya watoto njiti.
Kaimu mganga huyo,alitumia fursa hiyo kuwakumbusha akina mama wajawazito kujenga utamaduni wa kuanza mapema kuhudhuria kliniki ili endapo watagundulika wana tatizo,waweze kuhudumiwa mapema kabla tatizo husika halijaleta madhara makubwa.
Aidha, Kaimu Mganga Huyo Mfawidhi,amemshukuru Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwa kutoa msaada huo wa vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya watoto njiti.Amewataka wadau wengine kuiga kitendo hicho.
Kwa upande wake Miss Singida 2014, Dorice Mollel alisema amechukua hatua hiyo ya kusaidia watoto njiti kwa madai kuwa na yeye alizaliwa akiwa njiti pacha na kwa vyo vyote kuna watu walijitolea kuwasaidia katika kipindi hicho.
DSC03191Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida, Dk.Daniel Tarimo, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya tiba vilivyotolewa msaada na Miss Singida 2014 Dorice Mollel kwenye wodi ya watoto njiti hospitali ya mkoa wa Singida.
Aidha,alisema hatua hiyo ni kuiunga mkono serikali katika kupunguza vifo vya watoto wachanga nchini.Ametaka wadau wengine kusaidia kundi hilo la watoto ili kuwapunguzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wakati wa ukuwaji waoa.
Kwa mujibu wa Miss Singida 2014, Mollel baadhi ya vifaa hivyo ni suction mashine-manual na electronic na mizani vyote vina thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni.Mollel pia ni Miss kanda ya kati na alikuwa mshindi wa tatu katika shindano la kusaka Miss Tanzania la mwaka jana.
DSC03207Miss Singida 2014 Doris Moleli,akimwangalia mtoto mchanga aliyelazwa kwenye wodi ya uzazi kawaida iliyopo kwenye hospitali ya mkoa mjini Singida.
DSC03195Miss Singida 2014, Dorice Mollel akiangalia watoto njiti pacha waliolazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).

RIDHIWANI KIKWETE KUHARAKISHA MAENDELEO CHALINZE

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
 Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
 Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano  uliofanyika kijijini hapo
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo ambapo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero mbaalimbali walizonazo pamoja na suluhisho
 Ridhiwani akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika  Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa Serikali ya Kijiji cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana maendeleo ya wananchi badala ya maslahi yao binafsi.
 Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
 Ridhiwani akiifariji familia ya marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
 Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang’andu kinavyoteseka na kero ya maji.
 Mwanahawa Habib akielezea mbele ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho wanavyonyapaliwa na Daktari na wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
 Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang’andu
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwang’andu ambapo aliahidi kusaidiana na Ridhiwani kutatua tatizo la maji linalowakabili wananachi wa kijiji hicho
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo na kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya maji katika kijiji hicho cha Kwang’andu, Kata ya Mbwewe
 Mwananmke aliyejitangaza kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi Pili Mbwana akiomba mbunge Ridhiwani kusaidia kuwasaidia kupata mikopo  watu wanaoishi na VVU katika Kijiji cha Kunduchi Kata ya Mbwewe ili iwasaidie kuondokana na umasikini walio nao
 Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji kipya cha Kunduchi wakati wa ziara yake atika Kata ya Mbwewe jana
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao

 Ridhiwani akizungumza na Pili Mbwana anayeishi na virusi vya Ukimwi ambapo aliahidi kumsaidia jinsi ya kupata mkopo
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mkutano huo

MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA BARABARA YA MKAPA AWAMU YA PILI

unnamedMakamu wa Pili wa Rais Balozi Zanzibar Seif Ali Iddi akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Barabara ya Amani- Mtoni kwa awamu ya pili ya ujenzi wake katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. (kushoto alievaa kofia ya pama) Katibu Mkuu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Malik Akili. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. unnamed1Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuzindua Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni ikiwa ni shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar (kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. unnamed2Baandhi ya wananchi na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar. unnamed3Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribisha Balozi Seif Ali Iddi kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mkapa iliopo Amani-Mtoni Mjini Zanzibar. unnamed4Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika Sherehe ya uzinduzi wa Barabara ya Amani-Mtoni ikiwa ni miongoni wa shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. unnamed5Barabara ya Amani-Mtoni iliyozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

JENGO LATEKETEA KWA MOTO KARIAKOO

 Jengo la Ghorofa 8 likiwa linateketea katika ghorofa ya 4,Jengo hilo linamilikiwa na mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Haji Kube ,vitu mbalimbali zikiwemo Frem za Picha ,maua, vimeteketea kwa moto. ambapo mmiliki wa ofisi hiyo yuko nje kwa safari
 Wananchi wa kiliangalia jenjo la Ghorofa 8 lililokuwa likiteketea kwa Moto katika ghorofa ya 4  kwenye  Barabara ya Agrey maeneo ya Msikiti wa Kibla ten Dar es Salaa leo.
 Hapo wananchi wakikimbizana baada ya nguzo ya umeme kutowa mlipuko  katika Barabara ya Huru na Kongo Dar es Salaam  kama ilivyonaswa na mwandishi wa Jambo Leo alipokuwa akienda katika Jengo la Ghorofa 8 lililopo jirani na Msikiti wa Kiblateni .
Hapo wananchi wakikimbizana na kuondowa bidhaa zao baada ya nguzo ya umeme kutoa mlipuko  katika Barabara ya Uhuru na Kongo Dar es Salaam  kama ilivyonaswa  na Mmiliki wa Blog ya ujijirahaa, alipokuwa pilika zake za kazi

New Familiy Group yaomba kushirikiana na serikali kuhifadhi vijana wanaoleta hofu kwa wananchi

imagesKITUO cha New Familiy Group (NGFG) cha Mwasonga Temeke jijini Dar es Salaam kimeomba Serikali kushirikina na kituo hicho ili kuweza kuwahifadhi vijana ambao wanaonekana kuleta hofu katika Jiji wanaotambulika kwa jina la ‘Panya rodi’ ili waweze kulelewa kituo hapo.
Ombi hilo linakuja ikiwa ni siku moja vijana hao kutajwa kuwa wameibuka katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala na kufanya matokio ambayo yanahatarisha amani kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe Mwenyekiti wa NHFG Omari Kombe alisema kikundi hicho ambacho kinaundwa na vijana wengi wa mitaani kutoka mikoani kipo kwa muda mrefu lakini udhibiti wake umekuwa wa kusuasua.
Kombe alisema wamekuwa wakiwasiliana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto pamoja na Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia ili kwa pamoja waweze kupata muafaka wa tatizo hilo ila mwitiko kwa upande wa Serikali umekuwa duni.
“Unajua kwa muda mrefu vijana hawa wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya uhalifu na hili la jana ni endelevu lakini njia ambayo inaweza kuwa ni suluhisho ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo na eneo ambalo linaweza kuwapatia mafunzo ya ufundi, ujasiriliamali na mengine ambayo yatakuwa na tija nao,” alisema Kombe.
Kombe alisema NHFG ipo tayari kushirikiana na Serikali kwa kutoa eneo ambalo litajengwa kituo kikubwa mbapo watapata mafunzo hali ambayo inaweza kuleta amani kwa jamii.
Mwenyekiti huyo alisema NHFG ina eneo la heka 10 hivyo iwapo Serikali itaona ni jambo la msingi kujenga wao wapo tayari kushirikiana kwa maslahi ya vijana hao na nchi kwa ujumla.
Alisema iwapo vijana hao watashindwa kudhibitiwa kwa sasa ni ishara tosha kuwa nchi inatengeneza majambazi kwa miaka ijayo ambayo yatakuwa na uzoefu wa kutosha.
Kombe alisema vijana hao wameanza kutumiwa na kundi lingine la Mbwa Mwitu ambalo nalo limekuwa likiibuka kila mara katika maeneo  mbalimbali ya mji.
Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Serikali hasa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya uwepo wa panga rodi na mbwa mwitu yanaisha.

Abasi Kandoro awataka wananchi wa kudumisha amani

images Mwandishi Maalum
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka wananchi wa kudumisha amani kwani kinyume na uwepo wa amani hakuna maendeleo yatapatikana katika nchi na kwa wananchi. Kandoro amesema hayo wakati akizungumza katika mkesha wa amani ambao uliandaliwa na viongozi wa dini wa Mkoa huo kutoka makanisa mbalimbali.
Alisema amani ya Tanzania haiwezi kudumu  kama vitendo vya uvunjifu wa haki, uonevu, ukosefu wa maadili na ukosefu wa ajira vitaendelea kuongezeka katika jamii.
“Suala la amani ni la kila mtu katika jamii hivyo kinachohitajika ni kila mmoja wetu kuwa sehemu ya kuhakikisha amani inakuwepo kwa nguvu zoake zote,” alisema.
Kandoro aliwataka viongozi wa dini waache mahubiri ya kudai fedha zasadaka badala yake wafundishe waumini wao kufanya kazi kwa bidii ili mapato yao ndio watoe sadaka.
Alisema hivi sasa vijana wengi wapo vijiweni hawana kazi hivyo kinachohitajika ni juhudu kila mmoja wenu kwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha jamii iweze kukituma katika kujitafutia kipato cha halali badala ya watu kutoa sadaka za ufisadi, rushwa na madawa ya kulevya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo viongozi wa dini watasimamia haki taifa litastawi na kuwa mahali pa maendeleo na kuboresha uwajibikaji katika utumishi.
Akizungumza katika mkesha huo kwa niaba ya viongozi wa dini Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, alisema ni vyema viongozi wakazingatia maadili katika kutumikia Taifa na jamii ili kuondoa tabia ya ufisadi na rushwa iliozoeleka.
Mwamalanga alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa viongozi wa dini ambao wanawatetea watu ambao wamefaidika na fedha za Escrow waache kwani wanamkosea mungu.
Alisema mchakato wa kupiga vita ufisadi unahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo ni kosa kwa baadhi ya viongozi hasa wa dini kudiriki kutumia nafasi zao kutetea waovu.

Chamijata kuenda China Machi 28

indexMwandishi Maalum
CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) kimesema kimepata mwaliko kushiriki mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika nchini China kuanzia Machi 28 hadi 20 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chamijata Tanzania Mohammed Kazingumbe wakati akizungumza na Fullshangwe katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.
Alisema Chamijata imekuwaikipata mialiko mara kwa mara katika nchi za China na Korea Kusini hivyo kwa mwaka huu mwaliko wa kwanza ni kutoka China na mialiko mingine ipo ambayo ni kwenda Korea Kusini mwezi Septemba.
Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa wanahangaika kutafuta wafadhili ili waweze kupeleka timu na viongozi wa Chamijata wakati huo ukifika.
“Tumepata mwaliko wa kwenda China katika mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika Machi 28 hadi 30 hivyo jithada na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunashiriki,” alisema Kazingumbe.
Kazingumbe alisema Chamijata ina imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kuwa michezo ya jadi inarejea katika hadhi yake ya awali ambapo amewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha hilo.
Mwenyekiti huyo alisema Chamijata katika kuhakikisha kuwa inakuza mchezo huo itatumia kitabu ambacho wamekiandika chenye maelezo kwakina kuhusu mchezo wa bao.

Chamijata yapata msaada wa mabao kutoka kwa Diwani

indexMwandishi Maalum
DIWANI wa Kata ya Msongola Angelina Malembeka ametoa msaada wa mabao matatu kwa Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania (Chamijata) ikiwa ni jitihada zake za kuendeleza mchezo huo.
Malembeka ambaye pia ni Katibu wa Madiwani wa Manispaa ya Ilala alikabidhi mabao hayo jana katika ofisi za Chamijata zilizipo Temeke jijini Dar es Salaam.
Alisema ameamua kutoa msaada huo kwa Chamijata kutokana na kuona kwa muda mrefu mchezo huo umeshindwa kuvuma hivyo kwa kuanzia mabao hayo yatawasaidia.
Diwani huyo alisema pia katika kuendeleza mchezo huo amegawa mabao katika mitaa tisa ya Kata yake lengo likiwa ni kuendeleza mchezo huo kuanzia Mitaa hadi ngazi ya Taifa.
“Jamani naomba mpokee mabao haya ila naahidi kuendelea kuwasaidia pale msaada utakapo hitajika kwani mimi ni mdau  wa michezo hasa michezo ya jadi,” alisema Malembeka.
Malembeka alisema iwapo michezo ya jadi itapewa kipaumbele ni dhahiri kuwa jamii itadumisha tamaduni zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chamijata Gamaliel Mhanga alimshukuru Diwani huyo kwa msaada wa mabao hayo ambapo aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia chama hicho.
Mhanga alisema Chamijata imejipanga kutekeleza mipango yake mbalimbali ya kuboresha na kuendeleza michezo ya jadi kwa kushirikiana na wadau kama Diwani Malembeka.