MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abasi
Kandoro amewataka wananchi wa kudumisha amani kwani kinyume na uwepo wa
amani hakuna maendeleo yatapatikana katika nchi na kwa wananchi.
Kandoro amesema hayo wakati akizungumza katika mkesha wa amani
ambao uliandaliwa na viongozi wa dini wa Mkoa huo kutoka makanisa
mbalimbali.
Alisema amani ya Tanzania haiwezi
kudumu kama vitendo vya uvunjifu wa haki, uonevu, ukosefu wa maadili na
ukosefu wa ajira vitaendelea kuongezeka katika jamii.
“Suala la amani ni la kila mtu
katika jamii hivyo kinachohitajika ni kila mmoja wetu kuwa sehemu ya
kuhakikisha amani inakuwepo kwa nguvu zoake zote,” alisema.
Kandoro aliwataka viongozi wa dini
waache mahubiri ya kudai fedha zasadaka badala yake wafundishe waumini
wao kufanya kazi kwa bidii ili mapato yao ndio watoe sadaka.
Alisema hivi sasa vijana wengi
wapo vijiweni hawana kazi hivyo kinachohitajika ni juhudu kila mmoja
wenu kwa kushirikiana na Serikali kuhamasisha jamii iweze kukituma
katika kujitafutia kipato cha halali badala ya watu kutoa sadaka za
ufisadi, rushwa na madawa ya kulevya.
Mkuu huyo wa mkoa alisema iwapo
viongozi wa dini watasimamia haki taifa litastawi na kuwa mahali pa
maendeleo na kuboresha uwajibikaji katika utumishi.
Akizungumza katika mkesha huo kwa
niaba ya viongozi wa dini Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
Kipentekoste Tanzania, William Mwamalanga, alisema ni vyema viongozi
wakazingatia maadili katika kutumikia Taifa na jamii ili kuondoa tabia
ya ufisadi na rushwa iliozoeleka.
Mwamalanga alitumia nafasi hiyo
kutoa rai kwa viongozi wa dini ambao wanawatetea watu ambao wamefaidika
na fedha za Escrow waache kwani wanamkosea mungu.
Alisema mchakato wa kupiga vita
ufisadi unahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo ni kosa kwa baadhi ya
viongozi hasa wa dini kudiriki kutumia nafasi zao kutetea waovu.
No comments:
Post a Comment