Mbunge wa Jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa
(Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa
kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara
uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni
Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya
Bwilingu, Nasa Karama.
Muumini wa Dini ya Kikiristo,
Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Kikwete 9aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi
ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama
vyote jimbo humo hivyo ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote
wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa
uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.
Dok Rtaihwa akimkabidhi ufunguo
wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada
ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.
Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa ambulance
Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa
Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo
Wakiwa na furaha baada ya kuangalia samani zilizomo ndani ya ambulance hiyo
Ridhiwani pamoja na viongozi wa
dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji
Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula
Ridhiwani 9katikati) na Mbuunge
wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya
ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada
wa Ambulance na kuahidi kuitunza
Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo
Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo
Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya ambulance katika viwanja vya miembe saba mjini Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Mtera, Dodoma,
Lusinde ambaye alikuwa safarini akitokea Dodoma kwenda Dar kwenye vikao
vya Kamati za Bunge, aliamua kushiriki kwenye mkutano huo ambapo
alimsifia Mbunge Ridhiwani kwa kipindi kifupi alichoaguliwa kuwa mbunge
miezi sita iliyopita kutekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi alizozitoa
wakati wa kampeni ikiwemo ambulance hiyo, ujenzi wa visima katika vijiji
mbalimbali na ujenzi wa barabara pamoja na zahanati
Lusinde akikumbatiana kwa furaha na Ridhiwani baada ya mkutano huo kumalizika
No comments:
Post a Comment