Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifungua pazia
kuashiria ufunguzi wa wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika
Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka
51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo
Zanzibar). Sehemu
ya vitanda vya wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) katika Hospitali
Kuu ya Mnazimmoja. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wa tatu kutoka
(kushoto) akionyeshwa kifaa maalum cha kusaidia wagonjwa mahututi
wanapolazwa katika wodi hiyo. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo
Zanzibar). Waziri
wa Afya Rashid Seif akitoa taarifa juu ya wodi mpya ya wagonjwa
mahututi kabla ya kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
kuzungumza na walikwa katika hafla hiyo. Makamu
wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
wafanyakazi na wageni waalikwa katika ufunguzi wa wodi mpya ya ICU
katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya wakimsikiliza Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa ufunguzi wa wodi
ya wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo imefanya Hopitali Kuu ya
Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Maalim
Seif Sharif Hamad akiagana na Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja
Dkt. Jamala baada ya ufunguzi wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).(Picha
zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
………………………………………………………………………….
Na Miza Kona na Abdulla Ali –Maelezo Zanzibar
arif Hamad amewataka wauguzi
kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wabadilike kifikra na
mawazo katika kutekeleza majukumu yao.
Hayo ameyaeleza katika Hospitali
kuu ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa Ufunguzi wa Wodi
mpya ya Wagonjwa Mahututi (ICU) ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha
miaka 51 ya sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema wauguzi wana dhamana kubwa
ya kuokoa maisha ya watu hivyo wanajukumu la kuhakikisha wanatoa huduma
iliyo bora na ya uhakika.
Maalim Seif amesema wauguzi wa
wagonjwa mahututi (ICU) wana haki ya kupata mafunzo ili waweze kutoa
huduma hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu ili kufikia lengo lililokusudiwa.
“Wafanyakazi kuwa wapole, wenye
kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa, kuwa wastahamilivu na waliotayari
katika kutoa huduma zao”, amesema Maalim Seif.
Amewataka wafanyakazi wa ICU kuwa
wawazi katika kutoa taarifa zinazohusu maendeleo ya wagonjwa pale
inapohitajika ili kuondosha usumbufu kwa ndugu na jamaa wanapotaka
kupata taarifa hizo.
Aidha amewataka wananchi kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha usumbufu na matatizo zaidi kwa wagonjwa wa sehemu hiyo.
Maalim Seif amewataka wananchi
kutumia vyema huduma hiyo muhimu ili iweze kudumu na kupunguza gharama
za usafirishaji wa wagonjwa hao kufuata huduma nje ya nchi.
Mapema Waziri wa Afya Seif Rashid
Suleiman amesema huduma ya ICU ni muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya
watu na ni lazima ipate zana za uchunguzi za uhakika ili kuweza kufanya
matibabu ya uhakika na usahihi.
Amefahamisha kuwa Wizara imeandaa
mpango maalum wa kuratibu dawa zinazotumika nchini kupitia Bohari Kuu ya
dawa na Mfamasia mkuu wa serikali kuwacha kuagiza dawa zisizotumika ili
kupunguza gharama na hasara.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr.
Mohamed Saleh Jidawi amesema Wodi ya ICU ina vifaa vya kutosha na
huduma zote zinapatikana bila ya usumbufu katika wodi hiyo.
Wodi hiyo imegharimu zaidi ya Dola
millioni moja hadi kukamilika kwake ambayo ina vitanda nane na
inajitosheleza kwa huduma zote zinazohitajika kwa wagonjwa.
No comments:
Post a Comment