Mbunge wa Jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa
wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua
viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
Ridhiwani akisisitiza jambo
alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia
ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo,
Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa
mkutano uliofanyika kijijini hapo
Ridhiwani akihutubia katika
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo ambapo alijibu maswali
mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero mbaalimbali walizonazo pamoja
na suluhisho
Ridhiwani akizungumza jambo na
Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika Kijiji cha
Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe,
Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
Katibu wa CCM Wilaya ya
Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa Serikali ya Kijiji
cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana maendeleo ya wananchi
badala ya maslahi yao binafsi.
Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
Ridhiwani akiifariji familia ya
marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba baada ya kumalizika kwa
mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang’andu kinavyoteseka na kero ya maji.
Mwanahawa Habib akielezea mbele
ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho wanavyonyapaliwa na Daktari na
wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang’andu
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa
Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara
katika Kijiji cha Kwang’andu ambapo aliahidi kusaidiana na Ridhiwani
kutatua tatizo la maji linalowakabili wananachi wa kijiji hicho
Ridhiwani akihutubia katika
mkutano huo na kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya maji katika
kijiji hicho cha Kwang’andu, Kata ya Mbwewe
Mwananmke aliyejitangaza kuwa
anaishi na virusi vya Ukimwi Pili Mbwana akiomba mbunge Ridhiwani
kusaidia kuwasaidia kupata mikopo watu wanaoishi na VVU katika Kijiji
cha Kunduchi Kata ya Mbwewe ili iwasaidie kuondokana na umasikini walio
nao
Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji kipya cha Kunduchi wakati wa ziara yake atika Kata ya Mbwewe jana
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao
Ridhiwani akizungumza na Pili Mbwana anayeishi na virusi vya Ukimwi ambapo aliahidi kumsaidia jinsi ya kupata mkopo
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mkutano huo
No comments:
Post a Comment