Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la
Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo katika
wilaya ya Lushoto. akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya
mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na
wakulima wa Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya
kukirejesha kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi , Awali kiwanda
hicho kilikuwa kinamilikiwa na Mwekezaji Yusuf Mulla na kilifungwa
kutokana na mgogoro wa wakulima wa Chai na mwekezaji huyo . Rais Jakaya
Kikwete amechukua uamuzi huo baada ya katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Andulrahman Kinana kusikiliza kero hiyo ya wananchi wakati alipofanya
ziara ya mkoa wa Tanga na kuahidi kufuatilia ili kuhakikisha suluhisho
la kudumu linapatikana na wakulima hao wanapata haki yao. Mgogoro huo
umedumu kwa muda wa miaka kumi na kiwanda hicho kimefungwa kwa muda wa
miezi ishirini kabla ya Rais Jakaya Kikwete kufikia uamuzi wa
kukirejesha kwa wananchi. Msafara
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili katika eneo la
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mponde katika jimbo la
Bumbuli wilayani Lushoto. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akielekea kwenye eneo la Mkutano mara baada ya kushuka kwenye gari. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akisalimiana na Mwenyekiti wa Wakulima wa Chai Bw. Almasi Kassimu
ambaye alikuwa kiungo kikubwa katika kupatikana kwa suluhisho hilo. Baadhi ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye eneo la mkutano wa hadhara. Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Majid Hemed Mwanga akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kijiji cha Mponde mkoani Tanga. Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh. Mrisho Gambo akisalimia wananchi katika mkutano huo. Mmoja wa wananchi kijiji cha Mpond akipiga makofi huku akiwa amevaa sanamu Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Magalula Said Magalula akisalimiana na wananchi na kujitambulisha kwao kama mkuu wa mkoa huo. Mbunge wa jimbo la Lushoto Henry Shekifu akiwahutubia wanamponde. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akizungumza na wananchi wa na wakulima wa Chai Mponde wakati alipofika
kijijini hapo ili kuwataarifu juu ya rais Jakaya Kikwete kuamuru Kiwanda
cha Chai cha Mponde kurejeshwa kwa wananchi. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Injinia Mathias
Asenga aliyekuwa akiwaeleza wanachi juu ya kumalizika kwa mgogoro huo. Mbunge
wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akimshukuru Rais Jakaya
Kikwete kwa uamuzi wake wa kukirejesha kiwanda hicho kwa wananchi na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kushughulikia mgogoro
huo mpamka kufikia mwisho. Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba akiendelea kuzungumza na wananchi katika mkutano huo. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.
No comments:
Post a Comment