.BW. ALFREDY KAPOLE MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WA MWANZA AKIZUNGUMZA KATIKA MKOA HUO
WAANDISHI WA HABARI SHEILA SEZI NA GRACE CHILONGOLA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA MAMA YAKE NA PENDO
NYUMBANI KWAO NA MTOTO PENDO,
MWENYEKITI WA ALBINO MKOA WAMWANZA ALFREDY NA MWENYEKITI WA CHAWATA MKOA
WAKIONGEA NA MAMA PENDO EMMENUEL.
SUNGU SUNGU WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA VALENTINO MULOWOLA ALIPOKUWA AKITOA TAARIFA YA UCHUNGUZI HADI SASA
MKUU WA MKOA WA MWANZA MAGESA MULONGO AKIZUNGUMZA NA WANANCHI
…………………………………………………………………………………………
Serikali mkoani Mwanza imesema
hakuna kulala hadi mtoto Pendo Emmanuel (Albino) apatikane kufatia tukio
la kutekwa na watu wasio julikana toka tarehe 27.12.2014 katika kijiji
cha Ndami, Tarafa ya Mwamashimba Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza na kisha
kutoweka naye kwenda kusiko julikana hadi sasa.
MKUU WA MKOA.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo,
alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuwahusisha wananchi wakijiji hicho
pamoja na uongozi wa Wilaya na Mkoa huku akitaka kujua hatua
iliyofikiwa na wana nchi hao katika kuwabaini walifanya unyama huo.
Mtoto Pendo alitekwa na watu wasiojulikana mnamo usiku wa
tarehe 27.12.2014 majira ya saa nne usiku akiwa amelala na wazazi wake
huko Nyumbani kwao na kisha watekaji kutoweka naye na kwenda kusiko
julikana hadi sasa, huku taarifa za Polisi zikionesha jumla ya watu kumi
na watano (15), wakiendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa ajili ya
mahojiano zaidi.
Akihutubia wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
alisema ni tukio la kusikitisha kwani toka mwaka 2007 hakuna tukio la
namna hiyo lililo wahi kutokea katika Wilaya hiyo na tukio la mwisho
lililotokea lilimkumba mwananchi wa Wilaya hiyo aliyekuwa amesafiri
kwenda Mkoani Shinyanga kwa shughuli zake.
Amesema kiburi walicho nacho watekaji hakiwezi kuwa nje ya
mipaka ya kijiji hicho cha Ndami bali mpango mzima unajulikana kwa
wenyeji na ndio maana ilikuwa rahisi kufanya unyama huo “Kiburi cha
watekaji kimo humu humu haiwezekani mtu kutoka mbali aje atekeleze tukio
hapa kijijini bila yakuwa na wenyeji lazima kuna mtu au watu
walioshirikiana na wahalifu hao”, alisema Mulongo na kuongeza “ kwa
mazingira ya Nyumba ya kina Pendo ilipo kule hakuna sehemu yakutokea na
kama mliona pikipiki inaranda randa mchana,.. iweje mshindwe kuitilia
shaka? Hapana, hii haikubaliki! mimi nimekuja kuwaambia nataka Pendo
apatikane na sio vinginevyo, nawapa siku tano ijumaa nitarudi hapa
mniambie Pendo yuko wapi! Alisema mkuu huyo wa Mkoa akionesha
kusononeshwa na tukio hilo.
“Mbona mifugo inapo ibwa inapatikana”? Aliwahoji viongozi wa
sungu sungu na kusema haiingii akilini kusema wakati wa tukio la utekaji
sungu sungu wote walikuwa wamekwenda kula chakula na ndipo kadhia hiyo
ilipotokea, mkuu wa mkoa, alihoji kufatia kauli iliyotolewa na kiongozi
wa sungu sungu kuwa wakati wa tukio askari wote wa sungu sungu walikuwa
wamekwenda kula majira ya saa tatu na tukio kutokea saa nne.
MWENYEKITI WA ALBINO MWANZA.
Awali akielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo, Mwenyekiti wa
chama cha watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani hapa Alfred Kapole,
alisema inasikitisha kuona wanadamu wakiwauwa binadamu wenzao kama vile
wanyama bila hata woga na vyombo vya maamuzi vikishindwa kutoa hukumu
kwa wakati huku akielekeza lawama zake kwa mahakama na Mkemia Mkuu. “Mh.
Mkuu wa mkoa inasikitisha kuona miongoni mwa kesi 72 zilizokuwa
mahakamani, ni kesi 3 tu ndizo zilizokwisha kutolewa hukumu” alisema
Kapole, na kuongeza ingekuwa ni kesi ya Wabunge wameshindana kwenye
masuala ya uchaguzi ingekuwa imekwisha hukumiwa lakini kwakuwa ni
mlemavu wa ngozi, basi kupuuzia kumekuwa kwingi mno. Alisema kapole.
No comments:
Post a Comment