Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando
……………………………………………………………………………….
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma
mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi
walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya
uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo
vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo
hostel
Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa
huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema
“Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa
wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa
wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma
kwenye mtandao huduma hiii ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu
wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari
tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza
na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na
wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”
“Airtel tumeona ni vyema tuizindua
hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale
mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa
litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma
Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema
Mmbando
Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI
255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa
wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao
pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini
wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo
ambapo kiingilo chake ni BURE”
Kampuni ya simu za mkononi ya
airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao
wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili
kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko
vyuoni kufikia malengo yao.
No comments:
Post a Comment