Fainali
ya Michuano ya Michezo kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
imeshereheshwa na burudani kabambe kutoka kwa wasanii mbali mbali wa
muziki, lakini pia burudani kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi walioonyesha
vipaji vyao kutokana na kuwa na khari wakti wote wa kujieleza, kujibu
maswali ambapo wanafunzi mbali mbali wameweza kujipatia zawadi kutoka
Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel Tanzania, ambao ndiyo Wadhamini Wakuu
walioweza kufanikisha Shughuli hiyo, ambayo kwa Wanafunzi hao pia
ilikuwa ni kupata Timu za College zitakazoshiriki Ligi ya Dar es Salaam
inayoshirikisha pia Vyuo vya Pwani na Bagamoyo, Michuano ya Kutafuta
Timu za Vyuo ni Mpango unaoratibiwa na Kampuni ya Miss Demokrasia
Tanzania, iliyopewa dhima na wenye haki Miliki ya kuwa waamdaji wa
Michezo hiyo Kila Mwaka.
Vyuo
ambavyo Tayari vimefanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha
NACTE INTER COLLEGE Championship Mpaka sasa baada ya kushinda Michezo
yake kwenye Makundi kwa njia ya Mtoano, iliyofanyika kwenye viwanja
mbali mbali vya vyuo ikiwemo D.I.T, Shirika la Elimu Kibaha, Ustawi wa
Jamiii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Viwanja vya Mabibo Hosteli,
N.I.T na Bandari College, Wenyeji wameweza kuingia hatua ya pili pamoja
na timu za I.F.M, CBE, TRA,MUHIMBILI, COET,COSS,UDBS.
Wengine ni Mwalimu Nyerere Memorial Academy,Institute of Adult Education, Kilimanjaro Institute College, St. Joseph
College, Zoom Polytechnic College , Tanzania Institute of Accountancy (TIA,Njuweni Institute of Hotel, Catering &
Tourism Management, Bagamoyo College of Arts (TaSUBa), St. Mary Teachers College, na Dar es salaam City College (DACICO).
Zaidi
ya Vyuo mia nne 400 vilivyopata usjali wa NACTE Tanzania vilitakiwa
kushiriki michezo hiyo lakini kutokana na sababu mbali zilizowasilishwa
na vyuo baadhi yao hawataweza kushiki kwa mwaka huu kutokana na kile
walichosema Maandalizi ya kustukiza ambapo wamewataka waandaaji kutoa
taarifa mapema ili kila chuo kiweze kuwaandaa wachezaji kwa ajili ya
kushiriki huku vyuo vingine vikiwa havina wachezaji wa kuweza kushiriki.
Ratiba
ya Michuano hiyo inaanza April ambapo timu hizo zitacheza ligi ya
Nyumbani na Ugenini na itachuku siku 45 hadi kumalizika zikiwa ni siku
za wikiend kuanzia April mosi hadi Mey 24, sambamba na Vyuo vya Mikoa ya
Kanda ya Ziwa, kanda ya Kaskazini, kanda ya Kati, Kanda ya Kusini, na
Kanda ya Zanzibar zitashiriki Michuano hiyo na timu zitakazofanikiwa
kuibuka na Ubingwa kwa kila kanda zitakutana kutafuta Bingwa wa chuo bora katika michezo Tanzania(NACTE) (The best in sports college Tanzania).
(Picha na Mpiga Picha wa MIDETA Entertainment)
No comments:
Post a Comment