Tarehe
8 Machi, 2015 Tanzania itaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo
itaadhimishwa kitaifa mkoa wa Morogoro. Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya
Siku ya Wanawake mwaka 2015 ni “Usawa kwa Wanawake ni Maendeleo ya
Haraka kwa Wote”.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, itaadhimisha siku hiyo kwa kuandaa kongamano la
kitaifa litakalofanyika tarehe 6/03/2015 mkoani Morogoro sanjari na wiki
ya maonesho ya wadau mbalimbali yatakayozinduliwa tarehe 03/03/2015 na
kufikia kilele chake tarehe 8/03/2015. Lengo kuu la kongamano ni kujenga
jukwaa la majadiliano ya kina kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake
na usawa wa kijinsia.
Mada kuu nne zimependekezwa kuwasilishwa katika maeneo yafuatayo:
1. Ukatili wa kijinsia (intimate partner violence- Ukatili katika mahusiano)
2. Haki za wanawake/binadamu na mchango wa wanaume katika
utetetezi wa haki za wanawake (Kwa mfano, ubakaji, ukatili kwa watoto/
wasichana)
3. Hali ya Mtoto wa Kike (mf. Ndoa za utotoni)
4. Ajira salama na haki katika ajira,
5. Tathimini ya sheria na sera (dawati la jisia na polisi) na
6. Majadiliano ( panel discussion) kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto inakaribisha mwanajamii yeyote aliyetayari kuandaa mada
katika maeneo yaliyotajwa hapo juu, awasilishe muhtasari wa mada yake
(ikisiri, abstract) yenye maneno kati ya 300 na 500 kwa ajili ya
maandalizi ya kongamano hili muhimu. Siku ya mwisho ya kuwasilisha
maelezo hayo (abstract) ni tarehe 20/01/2015.
Waandishi ambao muhtasari wa mada zao utakubaliwa
watafahamishwa tarehe 20/01/2015 na watashirikishwa katika maandalizi ya
mada kamili tarehe 31/01/2015.
Maelezo ya mada (abstract) yatumwe kwa:
(i) Elizabeth Makawa: e_palelamakawa@yahoo.com – Simu No. 0655 975478
(ii) Dinah Enock: edinnah@yahoo.com – Simu No. 0766 070376
(iii) Judy Kizenga: kizengajudy@yahoo.com – Simu No. 0754 564414
Tangazo hili limetolewa na
Anna T. Maembe
Katibu Mkuu
05/01/2015
No comments:
Post a Comment