Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
kulia akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Bw. Jamhuri David Willium walipomtembelea ofisi kwake wakati wa ziara
ya Uhamasishaji kwa Vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo
Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
Mkuu
wa Wilaya ya Mwanga Bw. Shaibu Ndemanga akizungumza na wajumbe kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walipomtembelea ofisini
kwake kabla ya kwenda kuongea na vijana kutoka Wilaya za Mwanga, Same na
Moshi vijijini kuwahamasisha na kutoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo
ya Vijana leo Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
Mwezeshaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa
akitoa elimu kwa Vijana wa Mwanga, Same, na Moshi Vijijini kuhusu Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana wakati wa uhamasishaji wa Mfuko huo leo Mkoani
Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
Baadhi
ya Vijana kutoka Wilaya za Mwanga, Same na Moshi Vijijini wakifuatilia
kwa makini elimu iliyokua ikitolewa wakati wa uhamasishaji kuhusu Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana pamoja na mafunzo ya ujuzi na stadi za maisha
yaliyokua yakitolewa na wahamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo leo Mkoani Kilimanjaro Wilaya ya Mwanga.
Vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Amina Sanga
akitoa elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Vijana wa Wilaya
za Mwanga, Same na Moshi Vijijini leo Mkoani Kilimanjaro.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Vijana wametakiwa kujitambua na kuwa na fikra yakinifu na bunifu
ili kuweza kutatua matatizo yanayowalenga na kuweza kuwa na maamuzi
katika shughuli wanazozifanya.
Hayo yamesemwa leo na Mwamasishaji kutoka Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa wakati wa semina ya Vijana
kuhusu uhamasishaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mkoani
Kilimanjaro katika wilaya ya Mwanga.
Bibi. Riwa amewashauri vijana kutumia changamoto ya ukosefu wa
ajira kuwa fursa ya vijana kujishughulisha kwa kujiunga katika vikundi,
kusajiri vikundi hivyo na kuandika andiko la Mradi litakaowawezesha
kupata mkopo unaotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili waweze
kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na kuweza kuendeleza jamii
inayowazunguka.
“Vijana mnapaswa kutimiza wajibu wenu kwa kujishughulisha na
kuachana na zana potofu yakukaa mitaani mkisubiri kufanyiwa maendeleo na
serikali ni vyema mkajiunga katika vikundi imara na kufanya kazi kwa
bidii ili kuweza kujenga taifa letu kwani vijana ni taifa la leo”
amesema Bibi Riwa.
Akizungumza wakati wa semina hiyo Mkuu wa Kituo cha Vijana
Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele amewataka vijana kutokuwa na dhana
potofu ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kuwa umewaletea fedha nyingi
hivyo kuibua miradi mingi isiyokua halisi kwani lengo la mfuko huo ni
kuwasaidia vijana kuwa na umoja katika kusimamia na kutumia fedha hizo
kwa makini ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Shaibu Ndemanga ameishukuru
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuutuma ujumbe uliofika
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kutoa elimu ya uhamasishaji kwa vijana
kwani vijana wa Mwanga wanahitaji sana elimu hiyo na wao kama viongozi
wa Wilaya wanajitahidi kuwaelimisha vijana na kuwasaidia pale
wanapohitaji msaada kutoka kwao.
Akichangia wakati wa semina hiyo Bw. Musa Michumvu kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga amewapongeza wahamasishaji kutoa Wizara
ya Habari na kuomba elimu hiyo kwa vijana kuendelea kutolewa mara kwa
mara kwani vijana wanahitaji kuelimishwa ili waweze kuthubutu na
kujitegemea kwa maendeleo ya jamii na taifa.
No comments:
Post a Comment