Mwananchi
kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani
Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji
hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini
uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye
thamani ya shilingi bilioni 25.7.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima akizungumza na wanakijiji wa Nyanguge
wilayani Bariadi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme iliyowekwa na
REA. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo. Sehemu
ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme
vijijini katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani
Simiyu.
Sehemu
ya watoto kutoka katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa
mkoani Simiyu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme
uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.
Wananchi
wa kata ya Shishiyu wakinyanyua mikono juu kama ishara ya kuridhishwa
na utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA kabla ya
kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akihutubia wananchi wa
kata ya Shishiyu (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mradi wa
umeme.
Mtaalamu
kutoka kampuni ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye akitaja orodha ya
vijiji vilivyonufaika na mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA
Awamu ya Pili. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo.
Mbunge
wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda akimpongeza Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza
umeme katika jimbo lake.
Mbunge
wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto) akitafsiri hotuba ya
shukrani iliyotolewa kwa lugha ya kisukuma na mmoja wa wakazi wa kijiji
cha Shishiyu mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikata utepe
kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA
Awamu ya Pili.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye tisheti ya
kijani) akisoma maandishi kwenye jiwe la msingi mara baada kukata utepe
kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) Mbunge wa
Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto mwa Waziri) na mmoja wa
wakazi wa Shishiyu wakibonyeza kitufe kama ishara ya uzinduzi wa mradi
huo.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati aliyeshika
mtoto); Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (wa pili kutoka
kulia waliokaa mbele) na Diwani wa Kata ya Shishiyu wilayani Maswa Pili
Kidesela (wa kwanza kulia waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara baada
ya kumalizika rasmi kwa uzinduzi wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment