Naibu
Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akifungua
kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni
nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya
Mapinduzi ya Zanzibar. -Vijana
wadogo kutoka katika kituo cha Nyerere Shaolin Group wakionyesha
umahiri wa kuweza kupambana na uhalifu katika sherehe za Uwekaji wa jiwe
la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni
Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kamishna
wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar akitoa maelezo kuhusiana na Uwekaji wa
Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa
ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. -Katibu
Mkuu Wizara ya mambo yandani Mbaraka Abdullwakili akitoa hotuba na
kumkaribisha mgeni rasmi katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha
Polisi mbweni nje ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia
miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar. -Naibu
Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akitoa
hotuba katika Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje
ya mji wa Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.kushoto yake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo
yandani Mbaraka Abdullwakili na kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar
Hamdani Omar. Naibu
Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati Haji Mwadini Makame katikati
akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi katika
Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi mbweni nje ya mji wa
Zanzibar ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
…………………………………………………….
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar. 5/1215
Katika kufanikisha kuwafichua na kuwakamata wahalifu wa
vitendo viovu vya ujambazi na ubakaji kunahitaji ushirikiano mkubwa
kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wanaoishi katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa leo huko Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar
na Naibu Waziri wa Aridhi, Makazi, Maji na Nishati Haji Mwadini Makame
wakati wa uzinduzi wa kituo cha Polisi kijijini hapo.
Amesema Jeshi la Polisi liko tayari kufanya kazi na raia
wema katika maeneo yao kwa kuwafichua wahalifu na kuwatia hatiani kwani
wananchi ndio wanaoishi katika maeneo yanayofanyiwa uhalifu na kuwepo
uwezekano mkubwa wa kufanikisha kazi zao.
“Wananchi shirikianeni kuwafichua wanaofanya vitendo vya
uhalifu, ujambazi, uvutaji wa bangi na uuzaji wa madawa ya kulevya ili
kazi ya jeshi la polisi ya kuwatia hatiani iwe rahisi”, alisema Haji
Mwadini.
Aidha alisema kuwa kujengwa kituo cha Polisi katika eneo hilo
la Mbweni ni faraja kubwa kwa jamii inayoishi hapo kwani lengo kuu ni
kuwepo ulizi na usalama wa raia na mali zao hivyo alitaka kituo hicho
kutumike kwa maengo yaliyokusudiwa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame
akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa kituo hicho
kimejengwa kwa msaada wa mdau mzalendo ili kuwanusuru wananchi wanaoishi
maeneo hayo na vitendo viovu vya ujambazi na uhalifu.
Aliwaomba wananchi wanaoishi wa hapo kukitumia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuanzisha ulizi shirikishi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbaraka Abdul
Wakili alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuwa na changamoto nyingi za
kupambana na vitendo vya ujambazi, hata hivyo wameweza kufanikiwa
kuwadhibiti majaambazi.
Alisema kujengwa kwa kituo hicho ni mfululizo wa kujenga
vituo vyengine kwa daraja A na C katika maeneo ya Pongwe, Mbuyutende na
Jozani kwa Unguja.
Ameongeza kuwa wamekuwa wakijenga vituo pembezoni mwa fukwe
za Bahari ili kwanusuru watalii na wananchi wa maeneo hayo kwa kuwapa
ulizi wa uhakika.
Uzinduzi wa kituo cha Polisi Mbweni ni moja ya shamrashamra
za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya
1964.
No comments:
Post a Comment