MBUNGE
wa jimbo la Chalinze ,Bagamoyo mkoani Pwani ,Ridhiwani Kikwete amesema
hayupo tayari kufanya mipasho ya kujibizana na baadhi ya viongozi kutoka
upinzani, wanaokwenda kutukana na kubeza utekelezaji wa ilani ya
CCM,kupitia mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.
Amesema
yeye ni mbunge wa kufikiria kutatua kero mbalimbali zinazowakabili
wananchi wa jimbo hilo na sio kupoteza muda kwa kutukana majukwaani.
Akizungumza
mara baada ya kufanya ziara yake kata ya Mdaula ambako vitongoji vinne
vimechukuliwa na vyama vya upinzani katika uchaguzi uliopita,Ridhiwani
alisema ifikie hatua kwa viongozi wa vyama kuacha kutumia mikutano ya
wananchi kutoa matusi ama kejli kwa chama kingine na badala yake waseme
masuala yenye tija.
Ridhiwani
alieleza kuwa majukwaa ni moja ya fursa ya kueleza yale ambayo chama
husika inayafanya, kuyatatua kwa wananchi na malengo yao ndani ya jamii
na si kupoteza muda kubeza chama kingine ama kutoa dosari.
Alisema
viongozi wote pasipo kujali itikadi za kisiasa wanatakiwa kuzungumza na
wananchi kujua kero zao ,na namna ya kuzitatua badala ya kila kukicha
kuzungumzia chama kingine ambacho kinaonekana utekelezaji wake.
Aidha
Ridhiwani alisema ataendelea kuumiza kichwa kutafakari namna ya kupiga
hatua kimaendeleo kwenye jimbo lake pasipo kujali itikadi za kisiasa.
“Kwa
upande wangu,mimi,ni jukumu langu kusimamia na kushirikiana na wananchi
wote kutekeleza yale wanayoyataka kwa kutafuta wadau na kuisukuma
serikali kutekeleza kero
za wananchi ,na sitothubutu kuwa miongoni mwa wale ambao wanatenga
jamii anayoiongoza kwasababu ya kisiasa’alisema Ridhiwani.
Aliwaomba
wananchi kijumla na viongozi wa vyama vya upinzani walio katika maeneo
machache ya jimbo la Chalinze kusema kero zinazowakabili,kumshauri na
kumkumbusha kile atakachosahau ili waweze kushirikiana na hatimae kuinua
maendeleo ya jimbo hilo.
Mbunge huyo anaendelea na ziara yake jimboni Chalinze,na tayari alishatembelea baaadhi ya vijiji na vitongoji kwenye kata za Kibindu,Mbwewe,Ubena,Mdaula na Bwilingu.
No comments:
Post a Comment