Mbunge wa Jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha
Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya kikazi pamoja na
kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita
iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa na
matapeli katika jimbo lake la Chalinze.
Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi
Mkuu wa Miradi wa Mkoa wa Pwani
wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi umeme utakavyosambazwa katika
Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine Jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti mpya wa Serikali ya
Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru mbunge kwa ahadi
mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika kijiji hicho.
Ridhiwani akibadilishana mawazo
na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha
Fukayosi Jimbo la Chalinze.
Mwenyekiti mstaafu wa Kata ya
Fukayosi,Adam Masoud akimuomba Mbunge Ridhiwani kuhikisha anaweka
miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya katika Kijiji cha
Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya kuwashukuru kwa
kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuangalia jinsi ya
kuzitafutia ufumbuzi.
Mkazi wa Kijiji cha Mkenge,
Khamis Mwanga akielezea kero ya barabara ya Mwavi hadi Mkenge ambayo
alidai inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho hivyo kumtaka
Ridhiwani awasaidia kuijenge barabara hiyo ili iweze kupitika bila
matatizo katika vipindi vyote. Ridhiwani aliwajibu kuwa tayari barabara
hiyo imepata mkandarasi anayetarajia kuanza kazi katika siku chache
zijazo.
Katibu wa CCM Tawi la Mkenge,
Omar Seleman akimuomba Mbge Ridhiwani asaidie kumalizia ujenzi wa
msikiti wa Mkenge, Ombi ambalo alilikubali na kuahidi kupaua kwa gharama
zake.
Ridhiwani akijibu maswali mbalimbali ya wananchi wakati wa mkutano katika Kijiji cha Mkenge
Ridhiwani akikagua maendeleo ya
ujenzi wa msikiti wa Mkenge ambao ameahidi kuchangia mabati na mbao za
kupaua jengo hilo la ibada.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya
Fukayosi, Olnjurie Marigwa akihtubia katika mkutano uliofanyika katika
kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi
Masoud Fundikira akimuomba Mbunge
wao Ridhiwan, anzishe mashindano ya mpira wa miguu kuwania kikombe cha
Ridhiwani Cup ili kuendeleza michezo katika jimbo hilo. Ridhiwani
alilikubali ombi hilo kwa kuanzia kutoa misaada ya mipira na jezi katika
kila timu ya kata za jimbo hilo.
Ridhiwani akihutubia katika
Kijiji cha Mwavi ambapo aliahidi kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la
alilogawiwa Mkorea ili kijiji cha mwwavi kipate haki.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo
Kombo Kamote, akiwafunda viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwavi
waliochaguliwa hivi karibuni ili wawatendee haki wananchi.
Ridhiwani akihutubia katika
mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kidomole, ambapo aliwajia juu
anaowaita matapeli wanaouza ardhi katika Jimbo la Chalinze bila kufuata
sheria na utaratibu. Alisema kuwa hayuko tayari kuona hata heka moja ya
jimbo hilo ikikuzwa bila utaratibu.
Ridhiwani akiagana na Meya wa Morogoro, Amir Nondo ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo hilo la Chalinze.
No comments:
Post a Comment