CHAMA cha Michezo ya Jadi Tanzania
(Chamijata) kimesema kimepata mwaliko kushiriki mashindano ya kurusha
mishale ambayo yatafanyika nchini China kuanzia Machi 28 hadi 20 mwaka
huu.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa
Chamijata Tanzania Mohammed Kazingumbe wakati akizungumza na Fullshangwe
katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.
Alisema Chamijata imekuwaikipata
mialiko mara kwa mara katika nchi za China na Korea Kusini hivyo kwa
mwaka huu mwaliko wa kwanza ni kutoka China na mialiko mingine ipo
ambayo ni kwenda Korea Kusini mwezi Septemba.
Mwenyekiti huyo alisema kwa sasa
wanahangaika kutafuta wafadhili ili waweze kupeleka timu na viongozi wa
Chamijata wakati huo ukifika.
“Tumepata mwaliko wa kwenda China
katika mashindano ya kurusha mishale ambayo yatafanyika Machi 28 hadi 30
hivyo jithada na mikakati yetu ni kuhakikisha kuwa tunashiriki,”
alisema Kazingumbe.
Kazingumbe alisema Chamijata ina
imejipanga vilivyo ili kuhakikisha kuwa michezo ya jadi inarejea katika
hadhi yake ya awali ambapo amewaomba wadau kuwasaidia kufanikisha hilo.
Mwenyekiti huyo alisema Chamijata
katika kuhakikisha kuwa inakuza mchezo huo itatumia kitabu ambacho
wamekiandika chenye maelezo kwakina kuhusu mchezo wa bao.
No comments:
Post a Comment