Mbunge wa Jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi mjini Chalinze, Wilaya ya
Bagamoyo, Pwani jana, ambapo pamoja na kuwashuru kwa kumchagua, pia
alisema atatumia uanasheria wake kuwasaidia baadhi ya wakazi wa jimbo
hilo wanaonyimwa haki zao za msingi ikiwemo kuporwa ardhi.
Ridhiwani akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Masoko mjini Chalinze
Mkazi wa Chalinze, Bibi akitoa
malalamiko yake mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ya kudhulumiwa shamba
lake na watu wasiojulikana.
Mkazi wa Chalinze Methodius
Kaijage, akiuliza swali kuhusu alama za x zilizowekwa kwenye nyumba zao
kwa ajili ya upanuzi wa barabara ambazo alidai ni takribani miaka kumi
imepita bila kupewa fidia hivyo kusababisha kukosa maendeleo.
Sehemu ya wakazi wa Kata ya Bwilingu, wakiwa katika mkutano na mbunge wao mjini Chalinze.
Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kitongoji cha Chalinze Mzee wakati wa ziara ya kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao
Ridhiwani akimsalimia mmoja wa wazee wa Kitongozi cha Chalinze Mzee
Mmoja wa vijana wa Chalinze Mzee akiuliza swali
Mzee Ibrahim Koga akielezea mbele ya Mbunge asivyotendewa haki na Baraza la Kata ya Bwilingu la kuporwa ardhi yake
Mama mwenye Jamii ya Kimasai
Rehema Lazaro akilalamika mbele ya mbunge kitendo cha baadhi ya wananchi
kutoa lawama kwa wafugaji wote badala ya wafugaji wanaofanya vurugu kwa
kupeleka mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kuchafua visima vya
maji.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
No comments:
Post a Comment