Kiungo mchezeshaji wa Manchester City, Yaya Toure ameibuka na kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2014 Ushindi huo wa Toure unamfanya awe amechukua tuzo hiyo mara nne mfululizo.
Toure, 31, ameibuka mshindi katika sherehe za tuzo hiyo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Lagos Nigeria.
Raia huyo wa Ivory Coast
amewashinda mshambuliaji wa Borussia Dortimund raia wa Gabon,
Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama.
Toure ameingoza Man City kubeba
ubingwa wa England huku yeye akiwa amepachika mabao 20 na kuwa kiungo
mwenye mabao mengi zaidi England.
No comments:
Post a Comment