KITUO
cha New Familiy Group (NGFG) cha Mwasonga Temeke jijini Dar es Salaam
kimeomba Serikali kushirikina na kituo hicho ili kuweza kuwahifadhi
vijana ambao wanaonekana kuleta hofu katika Jiji wanaotambulika kwa jina la ‘Panya rodi’ ili waweze kulelewa kituo hapo.
Ombi hilo linakuja ikiwa ni siku
moja vijana hao kutajwa kuwa wameibuka katika Wilaya ya Kinondoni na
Ilala na kufanya matokio ambayo yanahatarisha amani kwa wananchi wa Jiji
la Dar es Salaam.
Akizungumza na Fullshangwe
Mwenyekiti wa NHFG Omari Kombe alisema kikundi hicho ambacho kinaundwa
na vijana wengi wa mitaani kutoka mikoani kipo kwa muda mrefu lakini
udhibiti wake umekuwa wa kusuasua.
Kombe alisema wamekuwa
wakiwasiliana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto pamoja na
Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia ili kwa pamoja waweze kupata
muafaka wa tatizo hilo ila mwitiko kwa upande wa Serikali umekuwa duni.
“Unajua kwa muda mrefu vijana hawa
wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya uhalifu na hili la jana ni
endelevu lakini njia ambayo inaweza kuwa ni suluhisho ni kuhakikisha
kuwa kunakuwepo na eneo ambalo linaweza kuwapatia mafunzo ya ufundi,
ujasiriliamali na mengine ambayo yatakuwa na tija nao,” alisema Kombe.
Kombe alisema NHFG ipo tayari
kushirikiana na Serikali kwa kutoa eneo ambalo litajengwa kituo kikubwa
mbapo watapata mafunzo hali ambayo inaweza kuleta amani kwa jamii.
Mwenyekiti huyo alisema NHFG ina
eneo la heka 10 hivyo iwapo Serikali itaona ni jambo la msingi kujenga
wao wapo tayari kushirikiana kwa maslahi ya vijana hao na nchi kwa
ujumla.
Alisema iwapo vijana hao
watashindwa kudhibitiwa kwa sasa ni ishara tosha kuwa nchi inatengeneza
majambazi kwa miaka ijayo ambayo yatakuwa na uzoefu wa kutosha.
Kombe alisema vijana hao wameanza
kutumiwa na kundi lingine la Mbwa Mwitu ambalo nalo limekuwa likiibuka
kila mara katika maeneo mbalimbali ya mji.
Alitoa rai kwa wananchi
kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Serikali hasa Jeshi la Polisi ili
kuhakikisha kuwa matatizo hayo ya uwepo wa panga rodi na mbwa mwitu
yanaisha.
No comments:
Post a Comment