Na Mwamvua Mwinyi,Bwilingu.
WANAFUNZI
wa shule ya msingi Maluwi,Mtambani,kitongoji cha Mdaula,kata ya
Bwilingu,jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,wanakabiliwa
na kero ya ukosefu wa vyoo suala linalowasababishia kwenda kujisaidia
maporini.
Wakati
huo huo walimu na wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa maji na kupelekea kufuata maji mtoni ambako maji yake sio
salama kutokana,nyakati za mvua kusomba vinyesi na uchafu mbalimbali
unaoingia mtoni humo.
Akizungumzia
kero hiyo ,juzi,shuleni hapo,mwalimu mkuu wa shule ya Maluwi,Shabani
Makuka alisema changamoto hizo sio za wanafunzi pekee bali hata walimu
wanashida ya vyoo kutokana na sasa wanatumia choo kilichojengwa kwa
nyasi.
“Shule
hii kijumla na wakazi wa Mtambani pia inakumbwa na kero ya ukosefu wa
huduma za kiafya hali inayosababishia kufuata huduma za kiafya Chalinze
ambako umbali wake ni km zaidi ya 15 kutoka Mtambani,na kwa wale
wanaoshindwa kwenda Chalinze uamua kumeza panadol za kununua bila
ushauri wa daktari”alisema Mwalimu mkuu huyo.
Aidha
Makuka alisema zipo changamoto nyingine ambazo ni pamoja na uhaba wa
madarasa,madawati na utoro mkubwa unaofanywa na wanafunzi hasa walio
jamii ya wafugaji ambao utoroka na kwenda kuchunga mifugo nyakati za
masomo.
Hata
hivyo Makuka alisema zipo hatua walizozichukua tangu ahamie kwenye
shule hiyo mwaka 2013 ambapo aliwaomba amjirani kuwa wakisaidia
wanafunzi hao kujistili pale inapobidi hasa kwa watoto wakike ambao
wamepevuka.
Pia walichangisha wananchi na kupata kiasi cha sh.1,200,000 na halmashauri ilitenga fedha na kuwapatia mil 2.5 jumla mil 3.7 ambazo wanatarajia kujenga choo kitakachosaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa choo shule hapo.
Changamoto
hizo zilifikishwa kwa mbunge mwenye dhamana ya kusimamia kero za
wananchi jimboni chalinze Ridhiwani Kikwete ambae alisema kitendo cha
kujisaidia maporini ni hatari kwa wanafunzi.
Ridhiwani
alisema atachukua hatua za haraka kuangalia namna ya kutatua kero
zilizopo shuleni hapo kwa kushirikiana na kamati ya shule na halmashauri
ya wilaya .
Shule ya msingi Maluwi imejengwa miaka 10 iliyopita,ina jumla ya wanafunzi 203,upungufu wa madawati 35 yaliyopo 45.
No comments:
Post a Comment