Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE
wa jimbo la Chalinze ,Bagamoyo mkoani Pwani ,Ridhiwani Kikwete amesema
hakugombea nafasi ya ubunge ili kuwa sehemu ya mapambio bali
aliitaka nafasi hiyo ili kuwa sehemu ya suluhisho katika kutafutia
ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Chalinze.
Alisema
kiongozi aliyeomba ridhaa ya uongozi kwa wananchi anapaswa kutimiza
ahadi alizozitoa na kutatua yale ambayo yapo ndani ya uwezo wake .
Aliyasema
hayo juzi,katika kijiji cha Changalikwa na Ng’andi kata ya
Mbwewe,Bagamoyo wakati akiendelea na ziara yake ya siku kumi anayoifanya
kutembelea kata mbalimbali jimboni hapo kujua kero za wananchi na
kueleza yale aliyoyatekeleza na kuyachukulia hatua pamoja na kuwashukuru
wananchi kwa kuichagua CCM katika chaguzi zilizopita za sekali ya
mitaa,vitongoji na vijiji.
Ridhiwani
alisema hayo baada ya kutolewa malalamiko hususan ya maji na kiafya
yanayowakabili kwa kiasi kikubwa wakazi wa kijiji cha Ng’andi na
Changalikwa.
Wakazi
hao walisema wanakabiliwa na tatizo la maji ambalo linawasababishia
kutumia maji ya kwenye mabwawa ambayo hayana usalama katika afaya za
watu na kufuata maji umbali wa km zaidi ya 5 huku wakinunua dumu la maji
kwa kiasi cha sh.500 hadi 700.
Kufuatia
kero hizo Ridhiwani alieleza kuwa hatotaka kuona anakuwa sehemu ya
pambio katika uongozi wake lakini atahakikisha anatatua kero kwa wananchi na kushirikiana nao kwa pamoja kwa lengo la kupata suluhisho la kero hizo.
Ridhiwani
alisema kwasasa anafanya taratibu ya kumpeleka waziri wa maji ili aweze
kwenda kutembelea maeneo yenye kero kubwa ya maji katika kata ya Mbwewe
hadi kata ya Kibindu, kujionea hali halisi ya uchungu wanaoupata
wananchi.
Alieleza
taarifa alishazifikisha kwa waziri husika na anaamini atafika katika
maeneo hayo ili aende kujua ukubwa wa tatizo hilo hatimae kulipatia
ufumbuzi na kuwaondolea changamoto hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inawapa
usumbufu wakinamama ambao wanatembea umbali mrefu kufuata maji.
“Nataka
kusema kwa undani kwa nguvu tunayokwenda nayo na nyie wananchi
kutafutia ufumbuzi matatizo mbalimbali mnayoyapata,naamini waziri
atakuja na atatusaidia kero hiyo “alisema Ridhiwani.
Ridhiwani
alisema atahakikisha kuyatekeleza yaliyo ndani ya uwezo wake
aliyoyaahidi katika muda mfupi wa uongozi wake ,na aliwaomba wananchi
kumkumbusha pale anaposahau na kushirikiana nae ili waweze kupiga hatua
ya kimaendeleo.
Alisema tayari alishakaa na viongozi wa mamlaka ya maji na kuzungumza nao ambapo
waliahidi kupatiwa maji kwa kujengewa vioski vitatu vya maji ambapo
kimoja kitakuwa katika eneo la shule Changalikwa na viwili vitakuwa
vijijini na kukamilisha tanki kubwa la maji lililopo Mbwewe ili kupeleka maji maeneo mbalimbali.
Aidha
alisema serikali bado inaendelea na hatua za kutatua kero hiyo ambapo
inachukua hatua ikiwemo kufanya upembuzi yakinifu na kuendelea na awamu ya tatu ya mradi wa maji wa WAMI ambao utasaidia kutatua kero ya maji jimboni hapo.
Akizungumzia suala la tatizo la kiafya matika maeneo ya Kibindu na Mbwewe Ridhiwani alieleza kuwa anaendelea kuzungumza na idara husika kuangalia namna ya kujazia watumishi wa afya katika maeneo yenye upungufu mkubwa na kupanga mikakati ya kujenga zahanati katika maeneo ambayo yana ukosefu wa huduma hiyo ili kuwaondolea adha wananchi wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za kiafya.
Akizungumzia suala la tatizo la kiafya matika maeneo ya Kibindu na Mbwewe Ridhiwani alieleza kuwa anaendelea kuzungumza na idara husika kuangalia namna ya kujazia watumishi wa afya katika maeneo yenye upungufu mkubwa na kupanga mikakati ya kujenga zahanati katika maeneo ambayo yana ukosefu wa huduma hiyo ili kuwaondolea adha wananchi wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma za kiafya.
Ridhiwani hadi sasa alishatembela kata 3 za Kibindu,Mbwewe na Ubena kwa kutembelea vijiji vinne kwa siku katika kila kata.
No comments:
Post a Comment