Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Rose Nyamubi (mbele) akizungumza na
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) pamoja na
watendaji wake waliomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara rasmi
katika mkoa wa Shinyanga. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mkoa huo
kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini
(REA) Awamu ya Pili pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya
wakazi wa wilaya ya Kishapu mara baada ya kuwasili wilayani humo.
Kushoto ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi
Wakazi
wa Kata ya Bubiki wilayani Kishapu wakimpokea kwa shangwe Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mara alipowasili wilayani
hapo huku wakiwa na mabango yaliyosomeka “ Profesa wa Kweli, Nchi sasa
inang’aa vijijini, Wewe ni Jembe”.
Mmoja
wa wakinamama kutoka kata ya Igubi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
akimfunga vitambaa mkononi Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo kama heshima kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza umeme
katika kata hiyo. Kata hiyo ni moja ya kata zinazonufaika na mradi wa
umeme vijijini unaotekelezwa na REA Awamu ya Pili
Mbunge
wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (katikati) akijumuika na wakazi wa
Kata ya Igumbi iliyopo wilayani Kishapu kucheza ngoma ya kumpongeza
Waziri wa Nishati na Madini kwa juhudi zake za kusambaza umeme katika
kata hiyo pamoja na jimbo lake.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Mbunge wa
Kishapu Suleiman Masoud Nchambi (kulia) wakifuatilia taarifa ya
utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na REA Awamu ya
Pili iliyokuwa inatolewa na Meneja Utaalamu Elekezi kutoka REA Gissima
Nyamohanga (hayupo pichani)
Mtaalamu
kutoka kampuni ya kusambaza umeme vijijini ya LTL (PVT) LTD Michael
Marenye (kushoto) akitoa taarifa ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa
miundombinu ya umeme katika wilaya ya KIshapu. Kulia ni Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo
alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Wakazi
wa Bubiki wilayani Kishapu wakimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) zawadi ya mbuzi wawili kama pongezi
kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme katika kata hiyo. Sehemu
ya umati wa watu kutoka Kata ya Bubiki wakishangilia hotuba ya Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
No comments:
Post a Comment