katikati), akiwa katika picha ya pamoja na timu yake. Kushoto kwake
ni: Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri na Mhe.
Kamishna Rehema Msabila Ntimizi. Na kulia kwake ni: Mhe. Kamishna
Kevin Mandopi na Mhe. Kamishna Salma Ali Hassan. Waliosimama kutoka
kushoto ni: Mhe. Kamishna Mohamed Khamis Hamad, Mhe. Kamishna Ali
Hassan Rajab na Katibu Mtendaji wa Tume, Bibi Mary Massay.
Sekretarieti ya Tume.
Massay wakimpongeza Mwenyekiti mteule wa Tume, Mhe. Bahame Tom
Nyanduga.
kuwapongeza na kuwakaribisha viongozi wateule.
hafla fupi ya kuwapongeza na kuwakaribisha viongozi wateule.
………………………………………………………………………………..
JANUARI 8 mwaka huu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora (THBUB), Bibi Mary Massay aliandaa hafla fupi kwa ajili
ya kuwapongeza na kuwakaribisha katika ofisi za Tume Mwenyekiti mteule wa Tume, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wapya.
Viongozi hao wapya walikula viapo vyao mbele ya Rais wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Ikulu jijini Dar es Salaam mchana wa siku hiyo. Nao ni: Mhe. Bahame
Tom Mukirya Nyanduga (Mwenyeketi), Mhe. Iddi Ramadhani Mapuri (Makamu Mwenyekiti) na Mhe. Mohamed Khamis Hamad (Kamishna)
Wengine ni: Wahe. Makamishna Kevin Mandopi, Rehema Msabila Ntimizi na Salma Ali Hassan.
Katika hafla hiyo viongozi hao wapya walipata fursa ya kufahamiana na wajumbe wa Sekretarieti ya Tume na pia Mwenyekiti Mstaafu wa Tume,Mhe. Amiri Manento.
Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Manento alisema kuwa amefurahi Tume
kupata viongozi wapya na hususan kumpata Mwenyekiti mwenye uzoefu
mkubwa katika masuala ya haki za binadamu. Aidha, aliwaasa viongozi
hao na wajumbe wa Sekretarieti ya Tume kutambua mamlaka (mandate) yao na kuyazingatia, kutojichanganya na siasa na kujitahidi wawezavyo kuitetea na kuiendeleza Tume. “CHRAGG is your mother, protect her at all cost,” alisema, akimaanisha kuwa pale mtu alipo au panapompatia riziki ndipo pake, hivyo ni budi apatetee na kupaendeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti mteule, Mhe. Bahame Tom Nyanduga alisema
kuwa wanatambua kuwa jukumu lililo mbele yao ni kubwa na kwamba
watakumbana na changamoto nyingi lakini anaamini kuwa kwa neema za
Mwenyezi Mungu watakabiliana nazo.
Alisema ili kuepuka lawama watahakikisha kuwa wanazingatia kiapo chao,ambacho ni moja ya misingi muhimu. “Naamini tutatenda kazi zetu kwa uhuru, bidii, haki, uaminifu, na bila upendeleo wala woga…kwa
kufanya hivyo tutakuwa tumeongeza thamani kwenye haki za watu wetu na hivyo kuleta amani nchini.
Chini ni picha za baadhi ya matukio katika hafla hiyo iliyofanyika
ukumbi wa mahakama, makao makuu ya ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment