Yote Uliyowahi Kutaka Kujua Kuhusu Mkito.com:
Mahojiano Na Mwanzilishi Mwenza,Sune Mushendwa
Kwa miaka nenda rudi, wasanii wa
kitanzania walikuwa na kilio kinachofanana. Ungekaa pembeni bila
kuwaona, ungedhani kutokana na mwangwi wa kilio chao, anayelia ni mmoja.
Hapana. Wote walikuwa [na pengine bado wanaendelea kulia] kutokana na
kunyonywa “jasho lao”.
Kimsingi “jasho” wanalolilia
limekuwa ni soko na usambazaji. Kipaji unacho na watu wanakubali kazi
zako. Tatizo utaifikishaje kazi yako kwa mashabiki zako? Ni wazi kwamba
unahitaji msaada wa kimasoko na usambazaji. Kusema utaweza kufanya kila
kitu peke yako ni kujidanganya.Nani? Yupo wapi na utampa kazi zako kwa
thamani gani? Kilio chao kilianzia hapo. Wengine wakaamua kuachana na
muziki [wengine muziki umewaacha wao] kutokana na ukosefu wa soko la
uhakika na kuona kadhaa ya kupanga foleni ukisubiri “hela yako”.
Mabadiliko ya masoko ya kazi za
wasanii duniani kutoka kwenye mifumo ya ki-analojia kwenda kwenye
dijitali na pia kutoka katika mifumo ya vitu kama CD mpaka kwenda kwenye
matumizi ya simu na vikabrasha vingine vya mikononi, kulimaanisha
kwamba soko la wasanii wa kitanzania [na Afrika kwa upana wake] lilikuwa
linazidi kufifia. Hakuna tena shabiki anayetaka kubeba furushi la CD.
Inakuwaje?
Hapo ndipo baadhi ya vijana
wakaona fursa kuthibitisha kwamba penye tatizo ndipo pa kukimbilia.Fursa
ni kama dhahabu au almasi.Huwezi kuiokota kando ya bahari ikiwa
imetupwa ufukweni na mawimbi ya bahari. Wazo la fursa likazaa Mkito.Com
mahali ambapo wasanii sasa wanapumua na huku changamoto pekee ni
kuwashawishi mashabiki kupakua kazi zao kutoka Mkito.Com. Kila mara
shabiki anapofanya hivyo, msanii ananufaika na kupata nguvu zaidi ya
kuingia tena studio kunogesha mambo. It’s a win win situation.
Sune Mushendwa [pichani juu] ni
mwanzilishi-mwenza wa Mkito.Com. Kujua mengi zaidi nilimtafuta na kupiga
naye story kidogo. Ameelezea mengi. Nakukaribisha usome mahojiano yangu
naye ili ujue yote ambayo umekuwa ukitaka kuyajua kuhusu Mkito.Com
.Twende pamoja;
BC: Sune karibu sana ndani ya
BongoCelebrity. Hii ni mara yako ya kwanza hapa na bila shaka wasomaji
wangependa kupata japo kwa kifupi tu historia yako. Ulizaliwa
wapi,ukakulia wapi na kusomea wapi na mambo kama hayo
SM: Asante sana kwa
kunikaribisha. Mimi nimekulia Arusha na ndipo niliposoma pia. Baada ya
sekondari nilienda kusoma chuo kikuu nchini Finland ambako mama yangu
ndipo anapotokea.
BC: Wajasiriamali wengi ambao
nimewahi kufanya nao mahojiano huniambia kwamba waliamua kufanya
wanachokifanya baada ya kukosa au kubughudhiwa na kitu fulani.Huwa kuna
kisa au mkasa nyuma ya pazia. Kwa upande wa Mkito kuna kisa au mkasa
wowote? Ilikuwaje mpaka ukasema Aha…Mkito ikaanza? Na hili jina lilikuja
namna gani?
SM: Baada ya
kutoka masomoni nilianzisha studio ya muziki Arusha.Lakini tatizo kubwa
lililoonekana moja kwa moja ni kwamba wasanii pamoja na studio zinapata
tabu sana katika kusambaza na kuuza kazi zao. Niliona tunahitajika njia
ya kuweza kusambaza muziki kirahisi na pia kuingiza kipato kwa msanii.
Baada ya research na maandalizi ya zaidi ya miaka 4 ndipo Mkito.com
ilipozaliwa tarehe 30 April 2014.
BC: Mpaka sasa Mkito imefanikiwa kuwa na wasanii wangapi? Nini masharti ya msanii kujiunga au kuweka kazi zake katika Mkito?
SM: Kuna wasanii
takriban 600 waliojiunga mpaka sasa na wanaongezeka kila siku. Masharti
ya kujiunga ni marahisi, uwe umerekodi wimbo anghalau mmoja wenye ubora.
Baada ya hapo msanii anaweza kujitengenezea akaunti yake kupitia tovuti
www.mkito.com na
kupakia[upload] nyimbo zake mwenyewe. Msanii baada ya hapo anaweza
kufuatilia mauzo yake mwenyewe kupitia akaunti yake aliyoitengeneza.
BC: Bado nikiwa katika swali au
maswali ya wasanii. Msanii akishaingia katika mkataba au makubaliano na
ninyi, bado anakuwa na haki na uhuru wa kuendelea kusambaza kazi zake
katika platforms zingine kama vile iTunes,Spotify,Google Play nk?
No comments:
Post a Comment