TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, January 8, 2015

MAKUNDI NDANI YA CCM CHANZO CHA UPINZANI KUCHUKUA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

imagesBULE
IMEELEZWA kuwa kitu ambacho kimewapa wapinzani nafasi ya kushika viti mbalimbali vya  madaraka hapa nchini ni kutokana na makundi makundi ambayo yamo ndani ya chama cha mapinduzi(CCM)
Hataivyo makundi hayo wakati mwingine husababisha hata kuyumba kwa chama hicho ambacho kina nguvu kubwa sana hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah Bulembo wakati akiongea na waandishi wa habari mapema jana Wilayani Meru mkoani Arusha.
Bulembo alidai kuwa makundi ambayo yamo ndani ya chama na hata nje ya chama yanachangia sana kuangamiza CCM na kutoa kipaumbele kwa wapinzani kusimamia mwanya huo kuwa CCM wao kwa wao hawapendani
Aliongeza, kuna umuhimu sasa wa wale waongozaji wa makundi ndani ya chama kuachana na tabia hiyo na kisha kuwa kitu kimoja ili kuweza kufikisha chama kwenye hatua ya juu ambayo inalengwa kufikiwa.
“wapo baadhi ya watu ambao wamebaki na kauli kuwa CCN klwa CCM hawapendani hili sio jambo la kufuraia hata kidogo na badaka yake tuwaangalia kwa namna hawa wanaosema hivi  kwani hawa ndio chanzo cha maanguko ya CCM”aliongeza Bulembo.
Akitolea Mfano Bulembo alisema kuwa kwenye jimbo la Arumeru Mashariki makundi pamoja na matatizo ndiyo yaliyochangia jimbo hilo kuwachukuliwa na Upinzani.
“napenda kusema kuwa makundi ndani ya chama sio kitu kizuri hata kidogo na makundi haya haya ndiyo yaliyosababisha Nasari kuchukua hili jimbo ila tumemuazima tu mwakani lazima tuhakikishe kuwa tunalirudisha”alisema Bulembo.
Naye kamanda wa vijana Wilaya hiyo ya Meru John Palangyo alisema pamoja na kuwa tayari ameshasimikwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa Wilaya hiyo atafanya michakato mbalimbali ya kuweza kutatua kero za vijana.

No comments:

Post a Comment