MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA NTALE MOSES (38) MKAZI WA AIRPORT
JIJINI MBEYA ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA
RUFAA JIJINI MBEYA KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA BAADA YA KUCHOMWA
KICHWANI NA KITU CHENYE NCHA KALI MNAMO TAREHE 27.12.2014 MAJIRA YA SAA
23:00 USIKU AKIWA NYUMBANI KWAKE HUKO AIRPORT.
MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MNAMO
TAREHE 05.01.2015 MAJIRA YA SAA 11:32 ASUBUHI HUKO KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA JIJINI MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. WATUHUMIWA
WAWILI 1. EZEKIA MENGO (23) MKAZI WA JAKALANDA NA 2. EZEKIA MWANSASU
(21) MKAZI WA AIRPORT WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.01.2015 MAJIRA YA SAA
06:00 ASUBUHI KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI
KATIKA SHULE YA MSINGI SAZA WILAYANI CHUNYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
EPANI RAPHAEL (10) ALIKUTWA AMEKUFA MAJI KWENYE KORONGO REFU LENYE MAJI
MENGI ALIMOKUWA ANAOGELEA NA WENZAKE.
MWILI WA MAREHEMU ULIPATIKANA
MNAMO TAREHE 05.01.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI
CHA KIBAONI, KIJIJI NA KATA YA SAZA, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA KIFO HICHO NI BAADA YA MTOTO
HUYO KUZIDIWA MAJI NA KUSHINDWA KUOGELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI TEULE YA MWAMBANI WILAYA YA CHUNYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WADOGO KWA KUTOA/KUWEKA UANGALIZI WA
KUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOWARUHUSU KUOGELEA KATIKA MITO, MABWAWA
KWANI NI HATARI KWA MAISHA YAO HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
TAARIFA ZA MISAKO:
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI AMBAO NI 1. ISACK MWAMPASHI (26) MKAZI WA
SAE- JIJINI MBEYA NA 2. DESDELIUS MZOGOLA (42) MKAZI WA IHANGA –NJOMBE
WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA SHOT GUN YENYE NAMBA CO 57126
ILIYOACHANISHWA, MTUTU UKIWA KWENYE BOMBA LA MAJI NA KITAKO KIMEFICHWA
KWENYE BEGI LA NGUO.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 04.01.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO ENEO LA MPAKANI- CHECK
POINT, KATA YA IGAWA, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA
WAKIWA KWENYE PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.173 CYJ AINA YA KING
LION WAKITOKEA MBEYA KUELEKEA NJOMBE VIJIJINI NYUMBANI KWA MMELU MGALA
MKAZI WA NJOMBE VIJIJINI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment