Wananchi na viongozi wa manispaa ya Iringa watakiwa kujitolea katika
maswala mbalimbali yahusuyo jamii kwa kuwajibika ipasavyo hasa katika
swala la kufanya usafi katika mazingira yanayotuzunguka.
Akizungumza na nuru fm mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa FRANK
KIBIKI amesema kuwa ameamua kufanya usafi katika maeno mbalimbali ya manispaa ya iringa kwa kuwa kikundi chao kimejitolea kufanya kazi hiyon
pamoja na kujitambulisha kwa uongozi wa halmashauri ya manispaa.
KIBIKI ameongeza kuwa kiongozi lazima uwe mfano kwa jamii husika katika kuleta maendeleo mbalimbali hasa kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua na kupenda kujifunza na kuijijali wao wenyewe hasa swala la usafi.
KIBIKI ameongeza kwa kusema kuwa kila mtu anayeishi duniani anaweza
kuzibzdili changamoto kuwa fursa ambazo zitakuwa na faida kubwa kwa
jamii husika lakini akasema kuwa sio kiasi gani cha fedha
alizizoziacha dunia buli ni familia gani ya familia aliyoiacha
duniani.
Aidha KIBIKI amewata wananchi wa manispaa kuwafundisha vijina jinsi
gani ya kufanya usafi hivyo watakuwa wamechangia kuioka jamii katika
swala afya kwa kuwa wananchi wote watakuwa wanajua umuhimu wa wa
kutunza mazingira.
KIBIKI amemalizia kwa kuwataka wananchi kuwa wasafi na kuwaridhisha
vijana kujua na kujifunza juu ya kufanya usafi hivyo usafi ukianzia
nyumbani basi hata mitaa yetu itakuwa misafi na tutakuwa
tumewatengezeza viongozi wazuri.
No comments:
Post a Comment