Watu waliokuwa wamejihami wameshambulia
ofisi ya jarida la vibonzo nchini Ufaransa Charlie Hebdo na kuwaua watu
12 huku wengine 7 wakijeruhiwa katika shambulizi linalodhaniwa kuwa la
kigaidi
Wanaume wawili waliokuwa wamefunika nyuso
zao waliwafyatulia risasi wahariri wa jarida hilo lakini walikabiliwa na
polisi ambao pia walifyatuliana risasi nao.
Wawili kati ya waliouawa ni maafisa wa polisi huku wengine waliojeruhiwa wakisemekana kuwa hali mahututi
Msako mkubwa unafanywa na polisi kuwasaka
waliohusika na uvamizi huo. Idadi ya wavamizi mwanzo ilisemekana kuwa
watu wawili tu lakini wizara ya ulinzi inasema inawasaka wavamizi watatu
Rais Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba waliofanya uvamizi huo waliokuwa magaidi.
Wachoraji wanne wa jarida hilo wanaosifika sana akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier waliuawa
Bwana Charbonnier aliyekuwa na umri wa miaka
47 aliwahi kupokea vitisho vya mauaji na tangu hapo amekuwa chini ya
ulinzi wa polisi
Hawa ni wachoraji wengine waliouawa katika
uvamizi uliofanyika ashubuhi wakati wa mkutano wa kila siku wa wahariri
wa jarida hilo
Baadhi ya waliojeruhiwa wanasemekana kua hali mahututi
Jarida hilo ambao hutolewa kila wiki,
limejikuta pabaya hasa baada ya kuwahi kumfanyia istihizai mtume
Mohammad wa dini ya kiisilamu picha ambazo ziliwakera sana waisilamu
Vyombo vya habari nchini Ufaransa
vimetahadharishwa na kutakiwa kuwa makini na maswala ya usalama hasa
baada ya tahadhari kutolewa kwamba nchi hio huenda ikashambuliwa na
wapiganaji wa kiisilamu baada ya matukio kadhaa ya kiusalama kabla ya
krismasi
No comments:
Post a Comment