Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman pamoja na Viongozi
wengine alipofika katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo kufungua jengo
jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) ikiwa
ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnanzi Mmoja Dk.Jamala Adam Taibu,alipofika
kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo leo
(Neurosurgical Unit) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kushoto) Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa taasisi ya ND kutoka Spein sherehe hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa
pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Mohamed Ali Haji (ustadh) wa
sehemu ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika
Hospitali ya Mnanzi Mmoja wakati Rais alipowatembelea wagonjwa mbali
mbali waliokwisha fanyiwa matibu na Kituo hicho baada ya kulifungua
jengo hilo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa
pilikushoto) na Makamo wa Kwanza wa Rais maalim Seif Sharif Hamad
wakipata maelezo kutoka kwa Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakilishi wa taasisi ya ND kutoka Spain wakati alipotembelea mashine za upasuaji baada ya kulifungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dk.Jamala Adam Taibu pia sherehe hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiwa mbele ya jengo la jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja baada ya kufunguliwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein likiwa la horofa mbili na uwezo wa vitanda 30 pamoja na vyumba (2)viwili vya upasuaji,[Picha na Ikulu.]
…………………………………………………………………………………
Na Miza Kona – Maelezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amekemea tabia ya baadhi
viongozi wa Taasisi kuwazuia wafanyakazi wake kujiendeleza kielimu kwa
lengo la kuongeza ujuzi na kuleta ufanisi.
Hayo ameyasema Hospitali kuu ya
Mnazi Mmoja katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji Vichwa maji na Uti wa
Mgongo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema tabia hiyo haifai kwani
inarejesha nyuma maendeleo ya wafanyakazi na kuanzisha majungu, fitna
na uhasama katika taasisi kati ya wafanyakazi wa kawaida na viongozi
wao.
Amefahamisha kuwa taaluma ndiyo
inayopelekea ufanisi bora wa kazi na kuleta mabadiliko kwa kutoa
huduma bora na uhakika na kujenga taifa lililo imara.
“Mabadiliko hayaji bila ya kuwa
na taaluma hasa katika sekta ya Afya hivyo viongozi waruhusuni
wafanyakzi wenu kupata elimu ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi”,
alieleza Dkt. Shein.
Amesema lengo la Serikali ni
kuipa hadhi Hospitali ya Mnazi Mmoja kuwa ya rufaa kwa lengo la
kuimarisha huduma bora lakini kutokana upungufu wa vitendea kazi
mabadiliko hayo yanakuja hatua kwa hatua.
Dkt. Shein ameeleza lengo la
Serikali ni kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kutumia
wataalamu wenye elimu na vifaa vya uhakika kadiri ya uwezo uliopo ili
kuimarisha afya za wananchi.
Aidha Dkt Shein amesema jitihada
kubwa zinahitajika katika kuandaa mipango madhubuti itakayosimamia
kuendeleza kitengo cha upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo kwa kutafuta
wataalamu na madaktari bingwa watakaoendesha matibabu hayo.
Amesema kitengo cha huduma ya
upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo ni cha pekee kwa Afrika Mashariki na
Kati ambacho kitasaidia kupnguza gharama za usafirishaji wa wagonjwa wa
matatizo hayo nje ya nchi.
Amesisitiza madaktari kuwafanyia
wagonjwa uchunguzi wa kina kabla ya kuwapa matibabu ili waweze kutoa
huduma ya uhakika na kujiepusha kubahatisha.
Aidha ameutaka uongozi wa
Hospitali ya Mnazi Mmoja kukamilisha sheria na kuweka taratibu ili
Hospitali hiyo iweze kujiendesha na kusimamia kazi bila kutegemea
Serikali kuu“Nijukumu la uongozi wa Hospitali
hii kuandaa mipango mizuri itakayoweza kuiimarisha ili lengo la
kujiendesha liweze kufanikiwa”. Alisitiza Rais wa Zanzibar.
Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi,
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman alisema kupatikana kwa miundombinu
katika kitengo hicho ni kuleta maendeleo katika sekta hiyo na ameeleza
kitatoa huduma ya uhakika Jengo hilo lenye vyumba viwili
vya upasuaji, wodi nne za kulaza wagonjwa na chumba cha mikutano
limejengwa kwa msaada wa Shirika moja la Hispania na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na limegharimu zaidi ya shilingi Mill 600 ambapo
asilimia 60 zimetolewa na wafadhili.
No comments:
Post a Comment